Social Icons

Loading...

TCRA yafungia vituo viwili vya redio nchini

KAMATI ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa adhabu ya kuvifungia muda wa miezi sita vituo viwili vya redio za dini, Imani na Kwa Neema kwa kile kilichoelezwa ni kuendesha vipindi vya uchochezi.Vilevile kamati hiyo imetoa adhabu ya faini ya Sh5 milioni kwa Kituo cha redio cha Clouds FM baada ya kubainika pia kukiuka taratibu za utangazaji kwa kurusha hewani kipindi kilichotafsiriwa kuwa ni cha uchochezi.

Kamati hiyo ya maudhui ilitangaza adhabu hizo jana jijini Dar es Salaam mbele ya waandishi wa habari ikisisitiza kuwa lengo lao ni kuhakikisha kuwa vyombo vya habari vinazingatia maadili.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya TCRA,Walter Bugoya alisema TCRA imefikia hatua hiyo baada ya kuyafanyia uchunguzi wa kina malalamiko yaliyotolewa na wasikilizaji wa vituo hivyo vya redio.

Bugoya alisema redio hiyo ilitangazia wasikilizaji wake wasishiriki kwenye mkakati huo wa Sensa ya Taifa kwa kile walichodai kulingana na imani ya Kiislamu, wasingejua hatima ya mkakati huo.
Kuhusu Redio Kwa Neema inayorusha matangazo yake kutokea Geita, Bugoya alisema ilieneza uchochezi dhidi ya mtafaruku wa kidini uliozuka mkoani humo juu ya upande gani una haki ya kuchinja wanyama kwa ajili ya kitoweo.

Akizungumzia Kituo cha redio cha Clouds, Buyoga alisema kamati imeitaka kulipa fidia ya Sh5 milioni baada ya kubainika kuwa nacho kilienda kinyume cha maadili ya utangazaji kupitia kipindi chake cha Power Break Fast, cha Jicho la Ng’ombe walitoa kauli za uchochezi.
Chanzo   gazeti  la  mwananchi

Real Madrid yaibamiza Barcelona 3 - 1 - Kombe la Mfalme.


Mbio za Urais 2015 - Watambue VINARA 9 wa URAIS,

WAKATI baadhi ya wanasiasa wakiwa wameanza kujiwinda kwa ajili ya kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, Shirika la Utafiti la Synovate limetoa matokeo ya utafiti wake ambao unaonyesha vigogo tisa kuwamo katika mchuano huo.Utafiti huo umeonyesha kuwa endapo uchaguzi huo ungefanyika sasa, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibrod Slaa angeibuka mshindi baada ya kuongoza orodha hiyo akipata asilimia 17.Katika matokeo ya utafiti huo uliofanywa Desemba mwaka jana, Dk Slaa anafuatiwa kwa mbali na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ambaye amefungana na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe kila mmoja akipata asilimia tisa.Hata hivyo, licha ya kuongoza, Dk Slaa ameporomoka kwa asilimia 25 ikilinganishwa na matokeo ya utafiti kama huo uliofanywa na taasisi hiyo mwaka 2011 ambapo alipata asilimia 42.

Kadhalika, umaarufu wa Pinda ambaye anaongoza miongoni mwa wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), umeshuka kwa asilimia tatu kutoka 12 za mwaka juzi, wakati Zitto ameendelea na kiwango kilekile cha asilimia tisa alizopata katika utafiti uliotangulia.Wengine wanaofuata na asilimia walizopata kwenye mabano ni Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli (8), Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa (7) na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba (5).

Pia wamo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (4) ambaye amefungana na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe (4) na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta (2).Ikilinganishwa na utafiti wa 2011, Lipumba ameporomoka kwa asilimia tisa.
Lowassa amepanda kwa asilimia sita, Dk Magufuli asilimia nne, Mbowe na Membe wamepanda kwa asilimia mbili kila mmoja, wakati Sitta amebaki katika kiwango kilekile cha asilimia mbili.
Hata hivyo, utafiti huo umeonyesha kuwa wananchi ambao hawana uamuzi wa kuchagua mtu yeyote kati ya hao kwa sasa ni asilimia 18, likiwa ni ongezeko la asilimia 12 ikilinganishwa na utafiti uliotangulia.

CCM yatamba
Katika utafiti huo, CCM kimeonyesha kuwa ni chama ambacho asilimia 52 ya wananchi wangependa kujiunga nacho, kikiwa kimepanda chati kwa asilimia moja kutoka asilimia 51 mwaka jana.
Kwa upande wa Chadema, wananchi ambao wanapenda kujiunga nacho imeshuka kutoka asilimia 35 mwaka 2011 hadi 31 mwaka jana.
Chanzo :  http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1704718/-/127gf8a/-/index.html

Miji yenye gharama kubwa duniani

MIJI ya Sydney na Melbourne ni miongoni mwa maeneo yanayotajwa kuwa na gharama kubwa zaidi za maisha duniani.Miji hiyo ambayo iko nchini Australia, imeingia katika nafasi ya tano bora.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Kitengo cha Kiintelijensia cha Uchumi Duniani (EIU), gharama za maisha katika miji hiyo imezidi hata miji ya Ulaya na Marekani.Bara la Asia na Australia lina miji 11 kati ya 20 iliyotajwa kuwa na gharama za juu za maisha duniani, huku miji minane ikitoka Ulaya na mmoja ukitoka America ya Kusini.Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na kitengo hicho, licha ya bara la Amerika ya Kaskazini kuwa na nchi maarufu na zenye uchumi wa juu, hakuna hata mji mmoja ulioweza kuingia kwenye 20 bora.Katika utafiti uliofanyika miaka 10 iliyopita kulikuwako na  miji sita kutoka barani Asia, 10 kutoka Ulaya na minne kutoka Marekani katika 20 bora kwenye orodha ya miji 131 yenye gharama za juu kwenye nchi 93 duniani.

SEMINA YA NENO LA MUNGU na Mwl Christopher Mwakasege.


Ziara ya Rais MWAI KIBAKI nchini.

Rais Mwai Kibaki wa Kenya  yuko  nchini    Tanzania  kwa   ziara  yake  ya   mwisho akiwa  Rais     na   kuwaaga  watanazania   kabla  ya  kuachia  madaraka  katika  uchaguzi  mkuu   utakaofanyika    mapema  Machi   2013.

Rais wa TFF amewataka wadau wa soka kuwa katika hali ya utulivu.

  Rais wa shirikisho la soka nchini TFF Leodger Chilla Tenga 
 =====

Rais wa shirikisho la soka nchini TFF Leodger Chilla Tenga amewataka wadau wa soka kuwa katika hali ya utulivu, katika kipindi hiki cha kuusubiri ujumbe wa shirikisho la soka duniani ambao utakuja nchini mwezi ujao kwa ajili ya kutatua sakata la uchaguzi wa TFF.

Tenga ametoa rai hiyo kwa wadau, baada ya hali ya utulivu wa soka kuingia dosari kufuatia kila mtu kusema lake baada ya kamati ya rufa ya uchaguzi inayoongozwa na Iddi Mtiginjola kuliengua jina la aliekua mgombea wa nafasi wa uraisi wa TFF Malali Malizi kwa kigezo cha kukosa sifa za kugombea.

Hata hivyo Tenga ametoa msisitizo kwa wadau wa soka nchini kutambua kwamba sakata la uchaguzi wa TFF katu halitochukua mustakabali wa maandalizi ya mchezo wa kuwani nafasi ya kucheza fainali za kombe la dunia ambapo timu ya taifa Taifa Stars itapambana na timu ya taifa ya Morocco mwezi ujao.

AC MILAN YAIZODOA BARCA 2 - 0 UEFA LEAGUE



UZINDUZI WA ALBAM YA NYIMBO.


Matokeo Kidato cha nne zaidi ya 60% wafeli .

MATOKEO ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika mwaka jana yametangazwa. Watahiniwa 240,903 sawa na asilimia 60.6 wamepata sifuri, huku wanafunzi 23,520 tu ambao ni sawa na asilimia 5.16 ndiyo waliofaulu na wengine 103,327 sawa na asilimia 26.02 wamepata daraja la nne.
Akitangaza matokeo hayo jana, Waziri wa Elimu Dk Shukuru Kawambwa alisema watahiniwa walikuwa 456,137, wa shule wakiwa 397,136 huku wa kujitegemea wakiwa 68,806.
“Matokeo ya mwaka huu yamekuwa mabaya sana, Serikali tunasikitika kutokana na hali hii lakini tuna mipango mbalimbali ya kuhakikisha tunaweza kutatua hili tatizo,” alisema Dk Kawambwa.
Dk Kawambwa alisema watahiniwa wote kwa ujumla waliosajiliwa walikuwa 480,036 kati yao wasichana 217,583 sawa na asilimia 45.33 na wavulana 262,453 sawa na asilimia 54.67 lakini waliofanya mtihani huo ni 456,137 sawa na asilimia 95.44, wengine 21,820 (asilimia 4.55) hawakufanya mtihani.
Fuatilia  zaidi  chanzo : http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1698112/-/11t0745/-/index.html
 

KP


Je Mghana kumrithi Papa Benedict wa 16

Kadrinali Peter Turkson
Kardinali Peter Turkson ambaye ni Mghana anatajwa kuwa miongoni mwa wanaoweza kumrithi Papa Benedikti wa 16 ambaye atajiuzulu mwisho wa mwezi huu. 

Iwapo Turkson atafanikiwa kuwa Papa, atakuwa mtu mweusi wa kwanza kushika nafasi hiyo ya ukuu wa Kanisa Katoliki.Moja ya mambo yanayozungumzwa kuhusu Kardinali huyo ni mtizamo wake kuhusu kukua kwa Uislamu duniani.

Licha ya kuongea lugha yake ya asili ya Fante na lugha nyingine za asili za Ghana, Kardinali Turkson anaongea pia Kiingereza, Kifaransa,Kitaliano,Kijerumani na Kiyahudi.Pia anafahamu Kigiriki na Kilatini.
'Mapapa watarajiwa wengine ni kama ifuatavyo:


                                 Kardinali Luis Tagle wa Ufilipino
                              Kardinali Angelo Scola wa Italia
                               Kardinali Christoph Schoenborn wa Austria
                                Kardinali Odilo Pedro Scherer wa Brazil
                                     Kardinali Ginafranco Ravasi wa Italia
                              Kardinali Peter Erdo wa Hungary
                              Kardinali Francis Arinze wa Nigeria.

Kardinali Joao Braz de Aviz wa Brazil

Je kuna ukweli katika hili ???


Majina ya kamati kuu ya CCM yapatikana.

HALMASHAURI Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi katika kikao chake cha siku mbili Februari 10 na 11, 2013 kilichofanyika mjini Dodoma kikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Mrisho Kikwete (pichani), pamoja na mambo mengine kimeridhia uteuzi na kufanya uchaguzi wa Wajumbe 14 wa Kamati Kuu yake.

HALMASHAURI Kuu ya Taifa ya CCM imeridhia uteuzi wa Dokta Salim Ahmed Salim kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu kupitia nafasi 10 za uteuzi wa Mwenyekiti wa CCM.

Wajumbe 14 waliochaguliwa kuwa wajumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ni:-

Wajumbe wa Kamati Kuu - Bara
1. Ndugu Pindi Chana
2. Ndugu Adam Kimbisa
3. Ndugu William Lukuvi
4. Dokta Emmanuel Nchimbi
5. Ndugu Jerry Slaa
6. Profesa Anna Tibaijuka
7. Ndugu Stephen Wassira

Wajumbe wa Kamati Kuu - Zanzibar.
1. Ndugu Shamsi Vuai Nahodha
2. Ndugu Hussein Mwinyi
3. Profesa Makame Mbarawa Mnyaa
4. Dokta Salim Ahmed Salim
5. Ndugu Maua Daftari.
6. Ndugu Samia Suluhu Hassan
7. Ndugu Hadija H. Aboud

John Mnyika: Sheria mpya zinawalinda mafisadi.

MBUNGE wa Ubungo Jijini Dar es Salaam (Chadema), John Mnyika amemtaka, Rais Jakaya Kikwete kutosaini marekebisho ya sheria mpya ya mabadiliko katika Sheria ya Ukaguzi wa Hesabu za Umma ya 2008.Mnyika pia anakusudia kukata rufaa juu ya uamuzi wa Spika wa Bunge, Anne Makinda kwa kutumia vibaya kanuni za Bunge kutokana na kitendo chake cha kuzivunja kamati tatu za Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) na Hesabu za Serikali Kuu (PAC).
 Akizungumza na Mwananchi Jumapili, jana, Mnyika alisema Rais Kikwete kabla ya kusaini marekebisho hayo ambayo yanaonyesha dalili za kuwalinda mafisadi, ajitokeze na kuwaeleza Watanzania faida na hasara ya mabadiliko ya sheria hiyo.
       Wiki hii Serikali iliwasilisha bungeni mapendekezo ya mabadiliko katika Sheria ya Ukaguzi wa Hesabu za Umma ya 2008, huku ikiongeza vifungu ambavyo vinapunguza nguvu ya Bunge katika kushughulikia taarifa ya Ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Soma  zaidi  : http://www.mwananchi.co.tz/habari/-/1597578/1689870/-/vlipm8/-/index.html

Man U, Chelsea, Arsenal Zang'ara EPL, City Wachapwa na Southampton

 Chelsea  4  Wigan  Athletic 1




Man U  2   Everton 0





Sunderland 0   Arsenal  1






Southampton 3  Man  city 1


  Matokeo  zaidi  :  BONYEZA  HAPA

  https://www.google.co.tz/#hl=en&output=search&sclient=psy-ab&q=epl+results&oq=epl++&gs_l=hp.1.0.0i3l3j0l7.2364.3455.1.7576.5.5.0.0.0.0.1354.5778.7-5.5.0...0.0...1c.a-nZOEjFEY8&fp=1&biw=1366&bih=568&cad=b&bav=on.2,or.r_gc.r_pw.r_cp.r_qf.

Nigeria wins AFCON 2013 , beats Burkina Faso 1-0


                                                   Team  manager   Steven  Keshi  


Utalii wa ngono waingia nchini.

KATIKA hali ya kawaida, tumezoea kuona watalii kutoka mataifa mbalimbali duniani wakija nchini kuangalia vivutio vya utalii vilivyopo.Baadhi ya vivutio hivi ni Mlima Kilimanjaro, mbuga za wanyama, majengo ya kale, mapango na nyumba za kihistoria.Hata hivyo, kumeibuka aina mpya ya utalii, unaojulikana kama utalii wa ngono, ambao unashamiri kwa kasi ukihusisha zaidi watalii wanawake wanaofuata wanaume wa Kitanzania hasa vijana.
        Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi Jumapili, unaonyesha kuwa utalii huo unaongezeka kwa kasi hasa katika maeneo yenye vivutio vingi vya utalii ikiwamo Arusha, Kilimanjaro na Zanzibar.
Imebainika kuwa katika utalii huu, wanawake hasa watu wazima walio na umri kati ya miaka 60 hadi 80 kutoka nchi mbalimbali, wamekuwa wakiingia nchini kwa lengo la kutafuta vijana wa kiume wa kustarehe nao.Uchunguzi huo unaonyesha kuwa wanawake ambao hawana vigezo vya uzuri vinavyopendwa na wanaume huko kwao, ikiwamo wembamba na urefu, husafiri kuja Tanzania kutafuta mwanamume atakayestarehe naye kingono.Hali hiyo inawakumba zaidi wanawake wanene, ambao kwa Ulaya hukosa wapenzi, hivyo kulazimika kusafiri kuja Afrika Tanzania ikiwamo kutafuta mwenza wa kustarehe nao.
Chanzo: http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1689836/-/11sei33/-/index.html

The World Most Powerful People.

Utafiti : Wanaotumia runinga kwa muda mrefu hupoteza nguvu za kiume.

WANAUME wanaotumia muda wa saa tatu na zaidi kwa siku kutazama runinga wanapoteza nguvu za kiume ukilinganisha na wale wanaotazama runinga mara chache.Utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Afya ya Umma cha Havard (HSPH) kilichopo Boston nchini Marekani, umebaini kuwa kuporomoka kwa kiwango cha mbegu za kiume kunahusiana moja kwa moja na kutofanya mazoezi na kutazama runinga kwa muda mrefu.
     Imeelezwa kuwa wanaume wanaotazama runinga kwa zaidi ya saa 20 kila wiki wanapoteza asilimia 44 ya mbegu za kiume ukilinganisha na wale wasiotumia muda mrefu katika runinga.Vilevile, wanaume wanaofanya mazoezi kwa zaidi ya saa 15 kwa wiki, wana uwezo wa kuongeza asilimia 73 ya mbegu zao ukilinganisha na wale wasiofanya mazoezi au wanaofanya mazoezi chini ya saa tano kwa wiki.
     Kiongozi wa utafiti huo, Dk Audrey Gaskin alisema mtindo wa maisha unachochea zaidi upungufu wa mbegu za kiume na uzalishwaji wa mbegu za kiume.Mtafiti huyo alifanya uchunguzi wa viwango vya mbegu za kiume za wanaume 189 wenye umri wa kati ya miaka 18 na 22 kuanzia mwaka 2009 hadi 2010.
Soma  zaidi :  http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1687952/-/11sd59u/-/index.html

Uingereza 2 Brazil 1 - Mechi ya kirafiki , Feb 2013


FAINALI AFCON 2013 NIGERIA VS BURKINAFASO

Nigeria  4     Mali  1


Ghana 1   Burknifaso 1  (  Penalt 3 - 4)

Google Celebrates Safer Internet Day.


Search giant Google is celebrating its 10th annual "Safer Internet Day" with the purpose of teaching people about their online rights and responsibilities, according to a report.
Google's theme for the year 2013 is called "Connect with Respect." The theme was built based upon the company's commitment to keeping people safe online. Google has created resources like Teach Parents Tech, Privacy Videos, Family Safety Center and Google Security Center to help netizens develop strong privacy and security habits.
      In addition, Google's Good To Know website, the company's biggest-ever consumer education campaign, offers privacy and security tips. It teaches people using the Internet the importance of 2-step verification, locking your computer when you step away, and making sure your connection to a website is secure.Furthermore, the Good To Know site also explains some of the building blocks of the Web like cookies and IP addresses. Technology can be sometimes confusing, and the industry often fails to explain clearly enough why digital literacy matters, says Google.
       Meanwhile, Alma Whitten, Director of Privacy of Product and Engineering at Google had this thing to say about the search giant's Safer Internet Day initiative:
"Protecting our users is one of our top priorities at Google. Whether it's creating easy-to-use tools to help you manage your information online or fighting the bad guys behind the scenes, we're constantly investing to make Google the best service you can rely on, with security and privacy features that are on 24-7 and working for you."Isn't it good to know that Google is at the forefront of making sure that the Internet should be free for everyone to use, while at the same time being vocal enough in reminding Web users to be cautious and responsible with their online activities? I believe we ought to give Google a lot of credit for doing so.
Source :  http://technorati.com/technology/article/google-celebrates-safer-internet-day/

Mhariri wa NIPASHE : Haikubaliki kuligeuza Bunge kibogoyo

Katika mkutano wa 10 unaoendelea mjini Dodoma tangu wiki iliyopita, umma umepigwa na butwaa kuingiwa na fazaa kubwa kutokana na mwenendo wa mambo ndani ya chombo hicho kikubwa na muhimu cha uwakilishi wa wananchi chenye wajibu wa kutunga sheria na kuisimamia serikali.
  Fazaa hii siyo ya bure ila ni kutokana ukweli kwamba ama kumekuwa na mbinu za kufanya chombo hicho kisitekeleze wajibu wake kupitia mbunge mmoja mmoja kwa sababu moja tu, ushabiki wa kisiasa ambao hauna tija. Huu ni ushabiki ambao tunathubutu kusema wazi kuwa unadimimiza siyo demokrasia tu bali pia umejikita kuilinda serikali isiwajibishwe ndani ya chombo hicho muhimu.

Wakati mkutano huu ukianza mjini Dodoma Jumanne Januari 29, mwaka huu, yaani wiki iliyopita, tulimkumbusha Spika wa Bunge kuwa ana mzigo wa viporo vya kazi ambazo ama alizitaka mwenyewe ziwasilishwe kwake kwa maamuzi, au wabunge walizipeleka kwake kwa maamuzi kutokana ama mambo kutokwenda sawa au kumtakiwa atoe maelekezo yake. Viporo hivi ni vingi na vipo tangu Bunge hili linaanza kazi mwaka 2011.
  Tulimkumbusha Spika juu viporo hivyo ili kuvitolea uamuzi, nia ikiwa ni kumkumbusha tu ili kwa kukaa kimya juu yake watu wasijekuanza kuhoji juu uimara wa kiti chake, uadilifu wa kuendesha shughuli za Bunge na utendaji wa haki kwa wabunge wote pasi na itikadi zao kwa kuwa wote wamechaguliwa na wananchi na wanatokana na mfumo halali wa kisiasa ambao taifa hili limeamua kufuata.
Tunajua mkutano wa sasa utaahirishwa Ijumaa hii, yaani keshokutwa, na inavyoelekea ni vigumu kwa maamuzi ya viporo vyote kutolewa maamuzi, lakini wakati viporo hivyo vikisumbua vichwa vya wananchi wengi huku wakihoji juu ya mwenendo mzima wa Bunge letu, mkutano huu umeshuhudia tena mambo ya aibu kubwa yakifanyika.
Ijumaa iliyopita, Jumatatu na jana, wabunge wamesema wazi mbele ya Spika kwamba kiti chake kinayumba, hakitendei haki kambi ya upinzani, kanuni za Bunge zinapindishwa ili tu kupotosha mambo, kuilinda serikali isiwajibishwe hali ambayo ni sawa na kusema kupora wajibu wa kibunge wa kuisimamia serikali.
Sakata la sasa lilianza na hoja ya Mbunge wa Kuteuliwa (NCCR-Mageuzi), James Mbatia, juu ya uadilifu wa sekta ya elimu ambayo ilikuwa nzito, yenye maana na ambayo kwa kweli ilikuwa inalenga kutafuta uwajibikaji ndani ya serikali juu ya mustakabali wa elimu ya taifa hili.
Kisha ikafuata ya Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika, ambayo ililenga pia kutafuta uwajibikaji serikalini katika suala zima la upatikanaji wa maji safi na uondoaji wa maji taka katika jiji la Dar es Salaam, huku mabilioni ya fedha yaliwa yemetumika bila kuwako kwa huduma yoyote ya maana ya maji, lakini pia ipo ya Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nasari, ambayo ilitaka kujielekeza kwenye suala la utendaji wa Baraza la Taifa la Mitihani. Kwa bahati mbaya sana hoja hii haikuwasilishwa kabisa, ni kama ikienguliwa juu kwa juu.

Kiti cha Spika katika sakata lote hili kinayooshewa kidole kwamba kimeshindwa kusimamia haki, kwamba kimeyumba kiasi cha kuegemea upande mmoja; ni hatari kubwa inapofikia hatua ya wabunge kwa ujasiri mkubwa wanathubutu kutuhumu kiti kuyumba kiasi cha kusababisha kukosekana kwa maelewano ndani ya Bunge.
Ni hatari kweli kweli!
Kwa wale walioangalia Bunge Jumatatu jioni watashuhudia walichokiona kwamba siyo taswira njema kwa taifa linalojitapa kuheshimu utawala wa sheria, demokrasia na kuheshimu kanuni, miiko na maadili yanaokubalika kijamii na kitaifa.
Kwa bahati mbaya sana tangu kuanza kwa Bunge la sasa mwaka 2010 kufuatia uchaguzi mkuu wa 2010, kumekuwa na hisia kwamba uimara wa kiti cha Spika umetiliwa shaka kubwa hasa katika suala zima la kutenda haki sawia kwa wabunge wote bila kujali wanatokana na chama gani cha siasa wanapowasilisha hoja zao.
Tunachukua wasaa huu kuweka wazi kwamba kama Bunge likigeuzwa kuwa sehemu ya muhimili wa utawala ama kwa dhahiri au hata kwa mlango wa nyuma ni wazi hakuna tena haja ya kuwako kwa chombo hicho, ni kwa maana hii tunamshauri Spika awe mvumilivu na asimame kidete kuhakikisha kwamba muhimili anaousimamia unatekeleza wajibu wake mkuu wa kikatiba kulingana na ibara ya 63 (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Mungano wa Tanzania wa kuisimamia na kuishari serikali ili iwajibike ipasavyo kwa wananchi wake. Yanayoendelea mjini Dodoma kwa sasa hakika ni juhudi za kutaka serikali ilale na kukoroma na wabunge waangalie tu. Hii haikubaliki na haitakubalika asilani.

CHANZO: NIPASHE

Tanzanians to Follow Education Conference Through Social Media

THE 8th eLearning Africa conference (eLearning Africa 2013) will this year be hosted by Namibia's Ministry of Education in conjunction with the Ministry of information communication technology (ICT) from May 29-31.The conference will be held in Windhoek, Namibia. In 2011, it was hosted by Tanzania. This year's international event will focus on tradition, change and innovation to show how new technologies combined with a pioneering spirit to improve lives are already changing the way people learn, work, and play.Tanzania Global Learning Agency (Ta- GLA) is one of the organizers of the conference and as it did in previous years, it will link Tanzanians to important sessions of the conference through technologies. The following are some of the key questions to guide discussions at eLearning Africa 2013: How are African youth shaping their identities and navigating different learning spaces with these technologies? Are new technologies fundamentally disruptive to tradition or do they open up space for the digitisation of tradition?
        How is innovation in Africa shaping the continent's learning landscape? Over 1,500 decision-makers and practitioners from the education, business and government sectors, with 80 per cent coming from Africa are expected to attend the international conference. A similar event was last year held in Cotonou, Benin, from May 23-25. It provided an opportunity for Tanzanians and other participants to explore and get exposure to best available educational technologies and practices in the world and a platform to profile the country worldwide.

Chinese language courses set to be offered at UDOM

University of Dodoma (UDOM) plans to offer Chinese language courses as a key to learning from the best practices of China. 
The courses will be offered under the newly established Confucius Institute at UDOM to allow students and ordinary citizens to learn and understand Chinese language and culture.
UDOM Vice Chancellor, Prof Idris Kikula revealed this recently in an interview on the university’s plans.“This will not only be beneficial to students but to all who wish to learn the language, especially businessmen who tend to travel to China,” said Kikula adding;
“We are very delighted that this plan has attracted many students as a large number have already registered for the course… the outcome has exceeded our expectations.”
According to Kikula, they have signed a memorandum of understanding for the establishment of the Confucius Institute at UDOM with Zhengzhou Institute of Aeronautical Industry Management (ZZIA) China to carry out the role.

Kibonzo


JK AZINDUA UJENZI WA UWANJA WA NDEGE KIGOMA

                 Rais   Kikwete  akizindua  ujenzi  wa  uwanja  wa  ndege     mkoani  Kigoma
Kwa  picha  na  taarifa  zaidi  tembelea
 http://issamichuzi.blogspot.com/2013/02/rais-kikwete-azindua-ujenzi-wa-uwanja.html

MTUKUTU SUPER MARIO BALOTELI ATUPIA 2 AC MILAN IKIIFUNGA UDINESE 2-1

Mshambuliaji   wa  Ac  Milan  Mario  Baloteli  akifunga  moja  ya  magoli  mawili  katika  mechi  yake  ya  kwanza  dhidi  ya  Udinese , Ac  Milan  iliinyuka  Udinese  2- 1.


KILELE CHA MAADHIMISHO YA MIAKA 36 YA CCM

 Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete akihutubia maelfu ya wakazi wa mji wa Kigoma na vitongoji vyake wakati wa kilele cha maadhimisho ya miaka 36 tangu kuzaliwa kwa CCM Mkoani Kigoma.










New Castle Yainyuka Chelsea ,Man U, Arsenal Zanawiri EPL

New  Castle  3  Chelsea  2


Man U  1  Fulham 0


Arsenal 1   Stoke  City  0



 Matokeo  zaidi    http://www.premierleague.com/en-gb/matchday/results.html

FOF Exposee Yafana sana - Princess Hall Sinza

FoF Xposee  ya  kwanza  mwaka  huu  imefanyika   kwa  mafanikio makubwa  katika Ukumbi wa Princes Hall Sinza ambapo kundi maarufu la Glorious Celebration, Amani Kapama, Bomby Johnson na Jesca Honore walinogesha  tamasha ,vyombo  vya  habari    kadha  wa  kadha  kama  Sibuka  Tv, Clouds Tv, wanahabari wa  kumwaga wa  mitandao  ya  kijamii (Bloggers)   walikuwepo ,Lengo  la   Friends On  Friday( FOF)  ni  kukutanisha  watu  wa  rika  , taaluma, vipawa  na background tofauti ili kujenga mitandao  ya  kibiashara, kijamii , kitaaluma  na  kiimani  na hufanyika  kila  ijumaa  ya  mwanzo  wa  mwezi   na  theme  ya  FOF  hii  ya  February  hii  ni  Vunja  ukimya ( FOF  Exposee) .

Exposee si chini ya Tano Zimefanyika , kama Ifuatavyo.

1. Mwanamuziki Jesca Honore ametangaza kuwa atazindua albam yake yenye jina la "Nimevunja Ukimya" Katika Ukumbi wa Serena Hoteli Katikati Ya Jiji la Dar-es-Salaam. Wakati huo huo Mwanadada huyo pia ali Xposee hadharani kuwa Mwaka huu mwezi wa tano atakuwa akifunga pingu za Maisha na Mtangazaji maarufu wa Channel Ten Boniface Magupa.

2. Mc Maarufu katika Jiji la Dar-es-Salaam Lawrance Mwantimwa ametangaza rasmi kufunga pingu za maisha na Mtoto wa Mchungaji Miss Wema lakini sio Sepetu, mapema mwezi wa April. Aki exposee Usiku wa Leo alieleza kuwa wamekuwa marafiki tangu mwaka 2001.

3. Kundi Maarufu la Glorious Celebration wame Exposee Usiku wa leo na kusema tarehe 24 February, 2013 wanatazamia kusheherekea miaka 2 tangu kundi hilo maarufu lizinduliwe rasmi katika Jiji la Dar. Mratibu wa Anniversary hiyo ya Glorious Mr. Prosper Mwakitalima ali exposee kuwa event hiyo itafanyika katika Kanisa la VCCT mbezi beach Kawe.

4. Mwenyekiti wa Friends On Friday Jijini Dar-es-Salaam, Papaa Ze Blogger ame Xposee usiku wa leo kwa kueleza anatazamia kuzindua kipindi kipya cha Tv katika Clouds Tv. Kipindi hicho cha Gospel Music and News kinatazamiwa kuanza rasmi mwezi huu wa pili.

5. Comedian Maarufu kama Mc Pilipili ame Xposee Usiku wa leo kuwa ameamua kuacha kazi ya Ualimu na Kuingia kwenye Comedian full time. Mc Pilipili alieleza kuwa ameamua kuachana na Chaki na Kuamua kushika Microphone mwanzo mwisho.
 Mwimbaji  maarufu  wa  nyimbo  za  injili  Jesca Honore  akitumbuiza .
 Amani  kapama  akiburudisha      FOF  Exposee
  Lawrence aki Exposee Usiku   huo.
Sehemu  ya  umati  uliohudhuria  usiku  wa  FOF.
   Wadau    wa  FOF   wakifurahia   jambo.
  Duu    Blogger  Daniel  akiwa  kati  na  waandaaji  wa  FOF
  Mdau maarufu  wa  FOF  Mwl  Mathew  Mndeme  akiwa  na   Bloggers
 Huyu  ni  Mc  Pilipili (Comedian   maarufu   hapa  Mujini ) akiburudisha-  Hapa  utacheka  mpaka  mbavu  ziume. 
   Mc    maarufu  Papa  Sebene    aka  Blogger Sam  Sasali  akimhoji    King  Chavala   "  Comedian  maarufu  "
Kundi Maarufu la Glorious Celebration  likitumbuiza   FoF  Exposee.

  Du  kuwafanya  watu  wacheke    ni kazi , cheki  Mc  Pilipili  alivyotoa  macho, huyu  bwana  anatisha     waweza  mtembelea    pia  kwenye  blog  yake  
  http://www.mcpilipili.blogspot.com


© Copyright Daniel Blog in Contemporary News
Back To Top