Social Icons

Loading...

FOF Exposee Yafana sana - Princess Hall Sinza

FoF Xposee  ya  kwanza  mwaka  huu  imefanyika   kwa  mafanikio makubwa  katika Ukumbi wa Princes Hall Sinza ambapo kundi maarufu la Glorious Celebration, Amani Kapama, Bomby Johnson na Jesca Honore walinogesha  tamasha ,vyombo  vya  habari    kadha  wa  kadha  kama  Sibuka  Tv, Clouds Tv, wanahabari wa  kumwaga wa  mitandao  ya  kijamii (Bloggers)   walikuwepo ,Lengo  la   Friends On  Friday( FOF)  ni  kukutanisha  watu  wa  rika  , taaluma, vipawa  na background tofauti ili kujenga mitandao  ya  kibiashara, kijamii , kitaaluma  na  kiimani  na hufanyika  kila  ijumaa  ya  mwanzo  wa  mwezi   na  theme  ya  FOF  hii  ya  February  hii  ni  Vunja  ukimya ( FOF  Exposee) .

Exposee si chini ya Tano Zimefanyika , kama Ifuatavyo.

1. Mwanamuziki Jesca Honore ametangaza kuwa atazindua albam yake yenye jina la "Nimevunja Ukimya" Katika Ukumbi wa Serena Hoteli Katikati Ya Jiji la Dar-es-Salaam. Wakati huo huo Mwanadada huyo pia ali Xposee hadharani kuwa Mwaka huu mwezi wa tano atakuwa akifunga pingu za Maisha na Mtangazaji maarufu wa Channel Ten Boniface Magupa.

2. Mc Maarufu katika Jiji la Dar-es-Salaam Lawrance Mwantimwa ametangaza rasmi kufunga pingu za maisha na Mtoto wa Mchungaji Miss Wema lakini sio Sepetu, mapema mwezi wa April. Aki exposee Usiku wa Leo alieleza kuwa wamekuwa marafiki tangu mwaka 2001.

3. Kundi Maarufu la Glorious Celebration wame Exposee Usiku wa leo na kusema tarehe 24 February, 2013 wanatazamia kusheherekea miaka 2 tangu kundi hilo maarufu lizinduliwe rasmi katika Jiji la Dar. Mratibu wa Anniversary hiyo ya Glorious Mr. Prosper Mwakitalima ali exposee kuwa event hiyo itafanyika katika Kanisa la VCCT mbezi beach Kawe.

4. Mwenyekiti wa Friends On Friday Jijini Dar-es-Salaam, Papaa Ze Blogger ame Xposee usiku wa leo kwa kueleza anatazamia kuzindua kipindi kipya cha Tv katika Clouds Tv. Kipindi hicho cha Gospel Music and News kinatazamiwa kuanza rasmi mwezi huu wa pili.

5. Comedian Maarufu kama Mc Pilipili ame Xposee Usiku wa leo kuwa ameamua kuacha kazi ya Ualimu na Kuingia kwenye Comedian full time. Mc Pilipili alieleza kuwa ameamua kuachana na Chaki na Kuamua kushika Microphone mwanzo mwisho.
 Mwimbaji  maarufu  wa  nyimbo  za  injili  Jesca Honore  akitumbuiza .
 Amani  kapama  akiburudisha      FOF  Exposee
  Lawrence aki Exposee Usiku   huo.
Sehemu  ya  umati  uliohudhuria  usiku  wa  FOF.
   Wadau    wa  FOF   wakifurahia   jambo.
  Duu    Blogger  Daniel  akiwa  kati  na  waandaaji  wa  FOF
  Mdau maarufu  wa  FOF  Mwl  Mathew  Mndeme  akiwa  na   Bloggers
 Huyu  ni  Mc  Pilipili (Comedian   maarufu   hapa  Mujini ) akiburudisha-  Hapa  utacheka  mpaka  mbavu  ziume. 
   Mc    maarufu  Papa  Sebene    aka  Blogger Sam  Sasali  akimhoji    King  Chavala   "  Comedian  maarufu  "
Kundi Maarufu la Glorious Celebration  likitumbuiza   FoF  Exposee.

  Du  kuwafanya  watu  wacheke    ni kazi , cheki  Mc  Pilipili  alivyotoa  macho, huyu  bwana  anatisha     waweza  mtembelea    pia  kwenye  blog  yake  
  http://www.mcpilipili.blogspot.com


author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright Daniel Blog in Contemporary News
Back To Top