MENU
HOME
Habari
Kingereza
Kiswahili
Biashara
Siasa
Michezo
Vichekesho
Vibonzo
Ujuzi
Technicals
Writtings
Contact Us
Daniel Blog in Contemporary News
Featured
Featured Posts
Post Title 1
Post Title 2
Post Title 3
Social Icons
Loading...
Home
»
Unlabelled
»
DARAJA LA MABATINI LAZINDULIWA
DARAJA LA MABATINI LAZINDULIWA
Rais Dk Kikwete alisema kufunguliwa kwa daraja hilo kumesaidia kumaliza kero ya ajali za kugongwa watu lakini pia msongamano umepungua na sasa TANROAD wanaendelea na upanuzi wa njia tatu kuanzia eneo la Natta hadi eneo la stendi ya mabasi Buzuruga.
“Tunzeni viwatunze na daraja hili litawezesha kulitangaza Jiji hili na Mkoa wa Mwanza hivyo ni vyema mkashirikiana katika utunzaji kwa wanaofanya uaribifu wa miundombinu yake ikiwa ni pamoja na kupitisha pikipiki, kuvunja taa na wengine kupanda na mawe kwa lengo la kuponda magari yanayopita chini hivyo vyombo vya ulinzi na usala vipo wachukulieni hatua kali,”alisisitiza.
Naye Waziri wa Ujenzi Dk John Magufuri alisema tayari Mkandarasi ameisha pewa kazi ya kusanifu daraja la kisasa na kubwa zaidi eneo la Furaisha ambapo Wizara imeisha toa fedha na litatumia shilingi bilioni moja ili kuwezesha eneo hilo kuwa na daraja pia.
“Tangu umeingia madarakani na kuona inafaa kukusaidia ambapo sikukuhonga ili unipe uwaziri bali kwa kuona inafaa zaidi, umeweza kujenga mtandao wa barabara za lami kwa kilomita 11,154 nchini kote ili kurahisisha watanzania kufika kila mahali hakika umetimiza wajibu wako kilichobaki ni kukuombea kwa mwenyezi mungu utakapo maliza muda wako na tutakukumbuka sana,”alisema.
Dk Magufuri pia alisema tayari Wizara yake imishatoa fedha kwenye Halmashauri ,mbalimbali nchini kwa ajili ya ujenzi wa barabara za vijijini ambapo Jiji la Mwanza limepata Sh. bilioni 1.1 na Manispaa ya Ilemela Shilingi bilioni 1.0.
“Nimshauri Mbunge Wenje auhudhulie vikao vya Baraza la Madiwani ili kupanga maendeleo badala ya kuhamasisha vijana kufanya maandamano na vurugu na kwa kupita kwenye barabara zilizojengwa na Rais Dk Kikwete, serikali ya CCM na hata kwa ujenzi wa daraja hili litasaidia kupunguza maandamano,”alisema huku akishangiliwa kwa nguvu kwa vijembe hivyo.
Aliongeza kuwa Mbunge Wenje leo amesema mwenyewe kuwa yeye si tikiti maji lakini inaonyesha kuwa ni tikitimaji kwani amekuwa na busara ya kuomba kwa serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kutambua hilo hata wenzake ndani ya CHADEMA kungelikiwa hakuna maandamano
.
Wali Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Ezekial Wenje, alipopewa nafasi ya kusalimia alianza kwa kuwapongeza wananchi, walimu, askari na watumishi wengine kwa kukatwa kodi na kufanikisha ujenzi wa barabara, daraja na huduma mbalimbali za kijamii.
“Bila wananchi kulipa kodi, bila kuchangia kununua bidhaa hakika hakuna ujenzi wa daraja wala barabara za kiwango cha lami hivyo ni vyema wananchi mkajipongeza kwa hilo kwani fedha zilizojengwa hapa niza kwenu na si za CCM,” na kushangiliwa na vijana wafuasi wa CHADEMA.
Wenje alisema kuwa nawapongezeni kwa kufanikisha kutokana na kulipa kodi zenu ambazo matunda yake mnayashuhudia leo lakini nikuombe Rais uweze kutujengea barabara ya kutoka Igoma hadi Buhongwa kwa kiwango cha lami yenye urefu wa kilomita 12.2 likiwemo daraja la Fumagila Igoma.
Meya wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Stanslaus Mabula akitoa salamu za jiji hilo alianza kwa kunukuu maandiko ya vitabu vitakatifu kuwa “watuwangu wanaangamia kwa kukosa maarifa” akimaanisha vijana kutumika vibaya na baadhi ya wanasiasa kwa kuwa mstari wa mbele kufanya maandamano na vurugu kwa matarajio makubwa.
“Maendeleo ni Mipango na Jiji la Mwanza, Mhe. Rais Dk Kikwete limekuwa likiitekeleza ikiwa ni Ilani ya CCM ya uchaguzi ya mwaka 2010 lakini kupita Baraza lake la Madiwani ambapo limejenga barabara za km 9 kwa bilioni 15.2 za lami, barabara za mawe km 2.9 kwa bilioni 1.6,”alisisitiza.
Aidha Halmashauri ya Jiji la Mwanza imeendelea na ujenzi wa vyumba 68 wa Maabara ambapo kila vyumba vitatu vinajengwa kwa kila sekondari moja ya Kata katika Kata 12 za Jimbo hili, Hlmashauri pia imetoa fedha za kusaidia ujenzi huo ambapo kila chumba kimoja imetoa shilingi milioni 20 na hivyo kila Kata itapewa milioni 60 kwa maabara tatu , awamu ya kwanza zimetolewa milioni 20.
“Tunatarajia ifikapo tarehe 21 Novemba tutakuwa tumemaliza ujenzi japo kuna baadhi ya watu na wanasiasa wanapita huko wakiwaambia wananchi wasichangie maendeleo lakini kiongozi mzuri ni yule anayewahamasisha wananchi wake anaowaongoza kuchangia shughuli za maendeleo ili kupatikana huduma bora za kijamii,” alishangiliwa na umati wa wananchi.
Awali Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Nishati) Charles kitwanga “Mawe matatu” Mbunge wa Jimbo la Misungwi alimpiga kijembe Mbunge Wenje kwa kusema kuwa vijana msitumike na sasa ni vyema mkajitambua kuliko kutumika kwani dunia ya leo niya Sanyansi na Teknolojia hivyo wajitambue ili kuendana na wakati.
“Acheni kutumika kwa maandamano na vurugu kwani havitawasaidia wala kuwaongezea maarifa hivyo ni vyema mkawa vijana wenye kuelezwa kisha nanyi mkachanganya akili za kuambiwa na zenu ili msiwe kama Bayuwayi,”alisisitiza.
This post was written by: Author Name
Your description comes here!
Get Free Email Updates to your Inbox!
Rss
Twitter
FaceBook
Google +
on Monday, October 13, 2014
Post a Comment
CodeNirvana
«
Newer Posts
Older Posts
»
Popular Posts
Mapishi:Supu ya Pweza kwa mama anayenyonyesha
WANAWAKE wengi hupata tatizo la kukaukiwa maziwa wanaponyonyesha. Tatizo hili husababishwa na mambo mbalimbali, likiwemo ukosefu wa vyaku...
JIPATIE KING'AMUZI CHA DIGITEK
Ofisi za mauzo ya DECODER za DIGITEK eneo la Makumbusho Dar. Blogger akikabidhiwa King'amuzi chake ch...
Higher learning institutions in TZ to adopt new automated registration system.
UCC - HQ Building . Higher learning institutions in Tanzania have for the first time adopted the academic registration information ...
Mswada kuhusu MAFAO uliowasilishwa na Mhe Mnyika
TAARIFA KWA UMMA Tarehe 03 Agosti 2012 kwa mujibu wa Kanuni ya 68 (7) ya Kanuni za Kudumu za Bunge na kwa kuzingatia kuwa mare...
Marufuku wanawake kukaa kiume kwenye pikipiki
Jiji moja nchini Indonesia ambalo limekuwa likifuata sheria za kiislamu maarufu kama sharia, liko mbioni kupitisha sheria ya kuwapiga ...
Utata Wagubika ARV Bandia
UTATA umegubika kuwapo kwa dawa bandia za kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi (ARV), baada ya ripoti ya Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFD...
Shule zetu na Kilimo cha Jembe la mkono.
Asante Bwana Yesu kwa hatua hii...
Jana tarehe 16 march 2014 katika ibada zote mbili katika kanisa la TAG Kinondoni Revival Church ( KRC ) mmliki wa blo...
Askofu Emanuel Lazaro wa TAG afungua kongamano la udhihirisho - Living Water Centre -KAWE
Bishop Emmanuel Lazaro aliyekuwa Askofu Mkuu wa Tanzania Assemblies Of God kwa zaidi ya Miaka 26 amefungua Kongamano la Udhihirish...
CBET Training Workshop- HQ
Categories
habari
siasa
technicals
vibonzo
vichekesho
© Copyright
Daniel Blog in Contemporary News
Post a Comment