Daniel header

Daniel header

ATCL

ATCL

Zuku

Zuku

nmbnw

nmbnw

Adverts

Tuesday, August 19, 2014

MAMBO YA BUNGE LA KATIBA .


PAPA AMRUHUSU PADRI TOKA TZ KUOA.

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis amekubali kumuondolea sakramenti ya upadri, Raymond Mosha wa Jimbo Katoliki la Moshi ikiwa ni miaka 20 tangu padri huyo aombe kuachana na daraja hilo.
Barua ya uamuzi wa Papa Francis ilisomwa juzi katika parokia na vigango vyote vya Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi katika ibada zilizofanyika katika makanisa ya jimbo hilo.
Miongoni mwa parokia ambazo barua hiyo ilisomwa ni Karanga ambako Paroko wake, John Matumaini alitoa tangazo hilo katika ibada zote. Uamuzi huo ambao ni nadra kutolewa na Papa, unamaanisha kuwa sasa padri huyo yuko huru kuoa na kuwa na familia.
Hata hivyo, wakati uamuzi huo ukitangazwa rasmi juzi, tayari Padri Mosha ambaye ni profesa wa falsafa na maadili katika Chuo Kikuu cha Nelson Mandela Arusha, ana mke na watoto watatu ambao kwa sasa wako vyuo vikuu.
Padri Mosha alisema aliandika barua kuomba kuondolewa daraja hilo mwaka 1994 kabla ya uamuzi kutolewa juzi.
Katika orodha ya mapadre 185 wa Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi iliyopo katika tovuti ya jimbo hilo, jina la Padri Mosha linaonekana likiwa ni namba 23.
Akizungumzia hatua hiyo, Padri Mosha alisema: “Ninafurahi kufunguliwa kifugo hiki na hii itanifanya niishi kama Mkristo. Kwa vile hawajaniondolea sifa ya kutoa huduma kama vile ibada za mazishi, sakramenti ya mwisho na ubatizo, nitaendelea kutoa kwa wahitaji kwa sababu ninaupenda ukristo.
“Nashukuru sasa nimekuwa muumini wa kawaida nitaweza kufunga ndoa kanisani kwa kuwa nilikuwa nimefunga ndoa ya kisheria tu kwa DC.”
Kuhusu kwa nini aliamua kuacha upadri, Profesa Mosha alisema ni baada ya kufanya kazi hiyo kwa miaka 20 na akaona ipo haja ya kuwa na familia lakini kanisa lilikuwa haliruhusu.
“Sasa kwa kuwa kanisa haliruhusu mapadri kuoa ndiyo maana nikaamua kuandika barua ambayo hata hivyo, imechukua muda mrefu kujibiwa na tayari nina watoto watatu wako chuo kikuu.

KP LEO


Monday, May 12, 2014

KP leo


DENGUE YAWA TISHIO DAR - Wachina 9 walazwa.


Wakati raia tisa wa China wakibainika kuugua ugonjwa wa dengue na kulazwa hapa nchini, Rais Jakaya Kikwete amevunja ukimya na kuagiza wizara zake mbili kukabiliana na ugonjwa huo kwa dharura.
Ugonjwa huo uliingia nchini tangu mwaka 2010 lakini mlipuko wake mkubwa ulibainika Machi mwaka huu na hadi jana wagonjwa zaidi ya 400 walikuwa wameambukizwa, huku watatu wakiripotiwa kufariki dunia, akiwamo Daktari Bingwa wa magonjwa ya akili, Dk Gilbert Buberwa anayezikwa leo, Dar es Salaam.
Rais jana aliziagiza Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na ile ya Fedha kushirikiana Bohari Kuu ya Dawa (MSD) kuchukua hatua za dharura kupambana nao kwa kuhakikisha vinapatikana vipimo vya kutosha na dawa.
Wachina walazwa
Taarifa kutoka Hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam zilieleza kuwa wagonjwa waliobainika kuugua homa hiyo hadi jana ni raia hao wa China na Watanzania wachache wenye historia ya kusafiri nje ya nchi hasa China, Ufilipino na Kusini mwa India.
Muuguzi katika kitengo cha magonjwa ya kuambukiza cha Aga Khan, Nyangee Lugoe alisema hospitali hiyo ilianza kupokea wagonjwa tangu Machi mwaka huu na kuanzia Aprili, raia wengi wa China wamegundulika kuwa na homa hiyo, ingawa baadhi walitibiwa na kuruhusiwa.
Agizo la Rais Kikwete
Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani huko Arusha, Rais Kikwete alisema: “Hili ni jambo la dharura la kitaifa lazima hatua muafaka zichukuliwe kudhibiti ugonjwa huu, ambao asili yake ni nchi za Asia na Bara la Amerika.”
Alisema dalili za ugonjwa huo ambao unasababishwa na mbu aina ya Aedes Egyptie anayeuma mchana ni homa kali ya kuumwa kichwa, maumivu ya viungo na kutoka damu puani na kwenye fizi na kupoteza fahamu.
“Napenda kutoa wito mtu yoyote ambaye atapata dalili za ugonjwa huu, aende mara moja hospitalini ili afanyiwe vipimo badala ya kunywa dawa,” alisema.
Tayari Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imetangaza kuanza kuchukua hatua za dharura kukabiliana na ugonjwa huo, ikiwa ni pamoja na uelimishaji na uhamasishaji wa jamii kuchukua tahadhari.
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Charles Pallangyo alisema jana kuwa wizara yake imetoa hadhari ya ugonjwa huo kupitia kwa waganga wakuu wa mikoa na wilaya kote nchini na itatoa mafunzo maalumu kwa watumishi wa afya ikiwajumuisha madaktari na mafundi maabara ili kuwajengea uwezo.

Tuesday, April 29, 2014

Champions League: Real Madrid humble Bayern Munich to reach final.

Real Madrid blew Bayern Munich away to reach the UEFA Champions League final with a 4-0 second leg victory which secured a 5-0 aggregate success.


Wednesday, April 16, 2014

KIBONZO


CARS FOR SALE - AT A THROW AWAY PRICE

 TWO CARS   FOR  SALE ...
 
 For serious buyer pls contact us via 0784717342   or mail:audaxmujun@yahoo.com; 
 
1. A SUZUKI SWIFT  IN AN IMACULATE CONDITION.

REGISTERED RECENTLY (APRIL 2014)
YEAR:2004
CC:1320
PRICE: 7.5M NEGOTIABLE
 
  
 
 
=========================================================================== 
 
2. AN IST CAR (ATTACHED) IN AN IMACULATE CONDITION, AT A THROW AWAY PRICE. 
  REGISTERED RECENTLY (MARCH 2014)
YEAR:2004
CC:1300
PRICE: 9.5M NEGOTIABLE
 
  
 
 
 FOR  SERIOUS BUYER KINDLY CONTACT us via 0784717342
 
 mail:audaxmujun@yahoo.com; 
 
 
 
 

PLUIJM ,TAMBWE WAKAMIANA .


Kocha  wa Yanga, Hans van Pluijm na mshambuliaji wa Simba, Amis Tambwe kila moja amejigamba kuhakikisha klabu yake inamaliza msimu kwa kupata ushindi katika mchezo  wa mwisho baina ya timu hizo.
Kocha huyo Mholanzi ameipongeza Azam kwa kutwaa ubingwa na kusema waliweka changamoto na presha kubwa hasa katika mechi zao za mwisho ambazo wote walikuwa wakipambana bega kwa bega kuusaka ubingwa.
Pluijm alisema anaipongeza Azam kwa kutwaa ubingwa huo na kudai mechi tatu ziliwaharibia baada ya kutoka katika michuano ya kimataifa.
“Hatuwezi kulaumiana kwa sasa, tunawapongeza Azam kwa ubingwa, lakini uzembe wetu umetugharimu kwa kushindwa kutumia nafasi tuliyokuwa nayo hasa baada ya kutoka katika Ligi ya Mabingwa Afrika.
“Tulikuwa na michezo mingi mkononi kuliko wapinzani wetu, lakini tukashindwa kujipanga jambo ambalo lilitugharimu na kufanya tucheze kwa presha kubwa  mechi za mwishoni  ili kuusaka ubingwa, lakini tambua kila timu ilijipanga hivyo tunakubali matokeo,” alisema.
Pluijm alisema sasa hivi wanaangalia mechi yao ya mwisho dhidi ya Simba ili waweze kuibuka na ushindi na kujipanga kwa ajili ya msimu ujao na Kombe la Shirikisho.
“Tuko Moshi  leo (jana) tuna mechi  ya kirafiki na baada ya hapo tutarudi Dar es Salaam kuweka kambi kwa ajili ya mechi ya mwisho ya ligi dhidi ya Simba Jumamosi, naamini tutashinda mechi hiyo na mambo mengine yatafuata,” alisema Pluijm.
Naye mshambuliaji wa  Simba, Tambwe amekiri timu yao haikuwa vizuri msimu huu, lakini hawatakubali kamwe wafungwe na Yanga Jumamosi ili kuwafariji mashabiki wao.
Mrundi huyo Tambwe alisema hapingani na maneno ya mashabiki wengi kuwa timu yao haikuwa vizuri msimu huu na ndiyo maana imeshindwa kutwaa ubingwa wala nafasi ya pili, lakini amedai kuwa  mechi ya Jumamosi afe kipa afe beki ushindi lazima.
Test  
Today 

BUNGE LA KATIBA LAOMBA KUONGEZEWA SIKU 60

Bunge Maalumu la Katiba limeomba kuongezewa muda wa siku 60 kuanzia Agosti 5, mwaka huu litakapokutana kwa ngwe ya pili.
Bunge hilo linahitimisha ngwe yake ya kwanza Aprili 25, mwaka huu likiwa limekutana kwa siku 67, kati ya 70 zilizokuwa zimetengwa awali.

Kwa muda huo wa ziada 60, iwapo wajumbe wote 629 watalipwa posho ya Sh300,000 iliyopangwa kwa siku, jumla ya Sh11.322 bilioni za walipakodi zitatumika ukilinganisha na Sh13.209 bilioni zilizotumika katika siku 70 za awali. Jumla ya fedha zote zitakazotumika kwa posho ni Sh24.53 bilioni, bila kuingiza gharama nyingine nje ya posho za wajumbe.

Jana, Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta alitangaza kwamba shughuli za Bunge hilo zitakoma wakati wajumbe wake watakapokwenda kusherehekea maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano, Aprili 26, mwaka huu.

Sitta alisema jana kwamba aliwasilisha maombi ya kuongezewa muda kwa Rais Jakaya Kikwete, ambayo yalikuwa hayajajibiwa.

Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue alipoulizwa jana alisema: “Mheshimiwa Rais (Kikwete) anachoafiki ni kama ambavyo kila mtu anaona mwenendo wa Bunge ulivyo, kwamba siku 70 haziwatoshi, hivyo alikubali kwamba wanahitaji kuongezewa muda. Ingawa mpaka sasa hajaamua atawaongezea siku ngapi, atakapoamua tutawafahamisha tu.”

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema alisema upo uwezekano mkubwa wa Bunge hilo kuongezewa siku 60 lakini akaongeza kuwa hilo litategemea bajeti itakayoidhinishwa na Serikali.i 5.
chanzo  fungua  link 

KWA HERI WINDOWS XP

Kampuni ya utengenezaji wa mitambo endeshi ya kompyuta (Operating Systems) ya Microsoft ilisitisha utoaji wa huduma za muda mrefu kwa mitambo ya XP, ni moja ya mitambo endeshi inayotumika na watu wengi sana.Tangu kutoka kwa taarifa hizo, kumekuwa na maneno na mikanganyiko mingi mno kwa wateja hususan hapa Tanzania.

Kwakuwa ni mitambo inayotumika kwa weingi kwenye kompyuta nyingi zinazotumika kwenye mabenki na maofisini, hivyo watu walifika mbali hata kusema eti pesa zetu hazipo salama tena. Hivyo, ili kuondoa hofu hizi zinazoizunguka jamii, ungana nasi Dudumizi kwenye kujua nini maana ya kikomo hiki cha huduma na jinsi gani kinaweza kuathiri biashara yako?

 Kwanini XP imefikia kikomo?

XP iliingia sokoni miaka 12 iliyopita, tangu kuingia kwake, imekuwa ni mtambo endeshi unaotumika kwa wingi na makampuni mengi duniani kote. Na pia ni moja ya mtambo endeshi kutoka Microsoft uliokaa kwa muda mrefu sokoni. Ingawa katika uhai wa Windows XP, kumekuwa na matoleo mengine mengi kama Windows Vista, Windows 7 na ya sasa ambayo ni Windows 8, lakini kampuni ya Microfost imeendelea kutoka msaada wa kiufundi na kimatumizi kwa wateja wake wote, hivyo kwa maneno mengine tunaweza kusema,muda wake wa maisha umefika na ni mzigo kiutendaji na hata kibiashara kwa Microsoft kuendelea kuhudumia Windows XP ndiyo maana wameamua kusitisha huduma kwa Windows XP.

Je nini maana ya usisitshwaji wa Huduma?

Hapa ndipo palitokea mkanganyiko miongoni mwa watu wengi, kusitishwa kwa huduma hakumaanishi kuwa kompyuta zote zinazotumia XP hazitotumika tena kama wengine walivyoifananaisha na uhamaji wa mitambo ya analog kwenda Digital. 

Kusitisha kwa huduma kwa XP kunamaanisha, kampuni ya Microfot haitoendelea kutoa huduma (Support) kwa watumiaji wa windows XP tena, huduma hizi ni kama masasisho (updates) ya kiusalama, maboresho ya ufanyaji kazi (kama vile XP SP1, 2..) na huduma nyongine za utumiaji.

Hivyo, unaweza kuendelea kuitumia XP bila shida kama una uhakika kukosa huduma hizo hakutoathiri biashara.

Je kama ninatumia Windows XP, kompyuta yangu itaendelea kutumika?
Jibu ni ndiyo ila kuwa makini. Kusitishwa kwa huduma kwa Windows XP hakumaanishi kuondolewa kwa XP toka kwenye kompyuta yako, bali ni kutoweza pata huduma, hivyo Windows iliyopo kwenye komputa yako itaendelea kutumika kama kawaida, ila kuanzia sasa uhakika wa usalama wako utaendelea kupungua siku hadi siku.
Chanzo  mtandao  wa  dudumizi

Sunday, April 13, 2014

KIBONZOSWALI? 
HAPA  NI  WAPI?  MVUA ZA  DAR  ZINAZOENDELEA  KUNYESHA  ....

MVUA ZALETA MAAFA DAR ES SALAAM.

Vifo, uharibifu wa mali, miundombinu na mafuriko, msongamano wa magari, baadhi ya wakazi wa jiji hilo kukimbia makazi yao, wengine kulala kwenye magari na nyumba za wageni vimewakumba wakazi wa Jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyake, kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha kwa siku ya nne mfululizo. 
  
Sehemu ya barabara iliyoharibika katika Daraja la Mpiji kwenye barabara ya Dar es Salaam Bagamoyo

Timu ya waandishi wa gazeti hili walifanya uchunguzi maeneo mbalimbali na kushuhudia hali halisi ilivyo, huku wanawake na watoto wakionekana kupata shida zaidi kwa kukaa nje ya nyumba zao, wengine kuhamia kwenye majengo ya shule.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam alisema jana kuwa walikuwa wakiendelea kukusanya taarifa za maafa ikiwamo vifo alivyosema ni vingi.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadik alisema kuwa yupo kwenye kikao na watatoa taarifa zaidi za maafa baadaye.

Kijana ambaye akufahamika jina lake akijaribu kuokoa maisha ya akina mama waliotaka kusombwa na mafuriko jijini Dar es salaam
 
Tegeta, Boko na Bunju
Mtoto anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka minne, amefariki dunia baada ya nyumba aliyokuwa akiishi kujaa maji na kushindwa kujiokoa kutokana na ulemavu, wakati mama yake akiwa kwenye shughuli za biashara.
Majirani wa mtoto huyo walisema tofauti na kawaida yao kumtoa mtoto huyo mvua inaponyesha, jana walimsahau na mama yake aliporejea alikuta maiti ya mtoto wake ikielea chumbani.
Katika mvua hizo takribani kaya 180 zimekumbwa na mafuriko huku wakazi wake wakijikuta hawana pa kwenda.
“Mimi nimekuwa hapa tangu Tanu imezaliwa, nyumba yangu imejaa maji nimeshazeeka sina mtu wa kunisaidia, wala sijui wapi nitakwenda. Nomba Serikali inisaidie,”alisema Hussein Ngaoma ambaye ni mjumbe wa nyumba kumi katika eneo hilo.
Naye Husna Ally ambaye pia nyumba yake imekumbwa na mafuriko alisema: “Nasikitika, maana nimepata hasara kubwa. Mimi ni mfanyabiashara katika eneo hili la Boko, nina duka la kuuzia samani limejaa maji na sijaweza kuokoa chochote. Mzigo wa Sh30 milioni umeharibika wote.”
Jeti Lumo
Katika eneo hilo licha ya kujaa maji, mfanyabiashara ndogondogo amefariki dunia kwa kusombwa na maji 

   Uukoaji  ukiendelea  .

Thursday, April 10, 2014

MDAU TOBI SHAURI MSHWAHILY APATA JIKO

Mdau   wa    blog na  forums   ya  JIACHIE    Mr  Tobi  Shauri   atimiza    ndoto  yake  muhimu  sana  ya  kupata  Jiko   , pichani  akiwa  na  mkewe  Bi  Angela   Tobi, kwa  niaba ya  blog  hii  nawatakia  KHERI  na  MAFANIKIO katika  maisha  yao  mapya  na mwanzo  mpya katika kila  jambo  mbele yao.

KP LEO


RAIS KIKWETE AWA BORA AFRIKA

Rais Jakaya Kikwete amechaguliwa kuwa kiongozi mwenye mchango mkubwa zaidi katika maendeleo barani Afrika kwa mwaka 2013.
Heshima hiyo kwa Rais Kikwete imetolewa na jarida la kimataifa la African Leadership Magazine Group na tuzo yake ilitarajiwa kutolewa jana jioni katika sherehe iliyopangwa kufanyika kwenye Hoteli ya St.Regis, Washington D.C, Marekani.
Taarifa iliyotolewa jana na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu ilisema kuwa tuzo hiyo ilitarajiwa kupokewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe kwa niaba ya Rais Kikwete.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, tuzo hiyo hutolewa kwa viongozi wa Afrika ambao hutoa mchango mkubwa wa kiuchumi na kijamii kila mwaka kwa watu wao, kama ilivyokuwa kwa Rais Kikwete kutokana na mwelekeo wake wenye mafanikio kwa masuala ya utawala bora.
Taarifa hiyo ilisema kuwa jarida hilo limetambua utawala bora chini ya uongozi wa Rais Kikwete ambao limesema umeifanya Tanzania kuwa nchi ya kupigiwa mfano na kituo cha uhakika cha uwezeshaji kutokana na mageuzi yaliyofanywa katika sera na mifumo ya uchumi.
Ilisema kuwa, Rais Kikwete alikuwa chaguo la kwanza la wasomaji wa jarida hilo ambao walipiga kura kupitia njia mbalimbali za mawasiliano za jarida hilo.
“Kuhusu maoni ya wasomaji wetu juu ya kiongozi yupi wa Afrika ambaye ni hodari zaidi kwa maendeleo ya kiuchumi na maendeleo, matokeo ya majibu ya swali hilo yamedhihirisha bila shaka yoyote kuhusu nafasi ya Rais Kikwete katika uongozi wa nchi yake,” taarifa ya Ikulu imelinukuu jarida hilo na kuongeza: “Ushahidi uko kila mahali, ameweza kusimamia uchumi ambao umekuwa kwa wastani wa asilimia saba kwa miaka yote ya uongozi wake.”
Chanzo  gazeti  la  mwananchi.

Thursday, April 3, 2014

HII NI KWELI ...


UEFA CHAMPIONS LEAGUE MADRID YAILAZA BVB 3- 0, CHELSEA YALALA 3-1 KWA PSG

MADRID  3     BVB  0


PSG 3    CHELSEA  1Taarifa   zaidi    soma  hapa
uefa champions issues

UTAFITI : WATANZANIA WENGI BADO TUNATUNZA FEDHA NYUMBANI .

Asilimia 70 ya Watanzania wanatunza fedha zao nyumbani badala ya mfumo rasmi ukiwamo benki na huduma nyingine za fedha, imebainika.
Hayo yamebainishwa kwenye ripoti ya FinScope iliyotolewa jana na Mfuko wa Kuendeleza Huduma za Fedha Tanzania (FSDT), ikionyesha kuwa benki nchini zimeongezeka na kufikia 50.

Utafiti huo uliohusisha watu 8,000 umeonyesha kuwa asilimia 70.4 ya Watanzania milioni 24.2 wanaostahili kupata huduma za fedha, hawazitumii kutokana na sababu mbalimbali.

Sababu hizo ni pamoja na ukosefu wa elimu ya masuala ya fedha, umbali kufikia matawi ya benki au wakala, gharama kubwa za uendeshaji wa huduma hizo, mazoea ya mfumo wa kijima wa utunzaji wa fedha, kukosa imani kuhusu usalama wa fedha zao.

Akizindua ripoti hiyo, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Benno Ndulu alisema jana kuwa pamoja na hali hiyo, kumekuwa na maendeleo makubwa katika sekta hiyo ukilinganisha na hali ilivyokuwa miaka minne iliyopita.
Soma  zaidi  mwananchi .