Social Icons

Loading...

Madhara Ya Mnara ya Simu Kwa Binadamu.

Teknolojia ya simu hutumia mionzi ya masafa marefu ambayo inajulikana kwa lugha ya kitaalamu kama “wireless microwave radation”, techinologia hii inaendelea kwa kadri siku zinavyozidi kwenda na watu wengi wanapendelea na kukimbilia kuishi sehemu zenye mtandao kwa sababu za urahisi wa kimawasiliano.

 Mawasiliano hayo ya simu usafiri toka sehemu moja kwenda sehemu nyingine kwa njia ya minara ya simu.  Sehemu yoyote ile ambayo unaoweza kupiga au kupokea simu tambua kunamtandao  unaosambazwa na minara hiyo.

Sehemu ambazo minara ya simu imeonekana kuwa na mionzi mikali zaidi ni milimani na kwenye miinuko nje ya miji. Mionzi hii ina madhara kwa binadamu,mimea na viumbe hai vingine kama wanyama sababu hupata dozi ya moja kwa moja  kutokana na kukosekana kwa vizuizi”  obstruction/ barriers” hali inayofanya mionzi kusafiri moja kwa moja kutoka kwenye chanzo hadi kwa viumbe hai, na hii hupelekea  kiwango cha dozi ya mionzi kuwa kikubwa  kwa muda mrefu.

Mionzi hii inauwezo wa kusafiri katika  umbali wa kuanzia mile 2 katika miinuko hadi miles 45 katika sehemu zenye vizuizi vichache(barrier) na ina uwezo wa wa kupenya hata kwenye ukuta na chuma. Minara hii inakuwa ni hatari zaidi endapo itatoa mionzi zaidi ya 1900 MHz. na hii imeonyesha kuwa na athari kwa viumbe hai wakiwemo banadamu wanaoishi ndani ya kilometa moja kutoka kwenye chanzo.

Pamoja na hayo  ni vigumu kukimbia mionzi hiyo sababu ipo kila sehemu yenye mawasiliano japo nguvu ya dozi inapungua kulingana na umbali wa chanzo na watu,, kuwepo kwa vizuizi kama vile majengo ambayo yanauwezo wa kupunguza nguvu ya mionzi hiyo na kupunguza muda wa dozi husika.


Aidha tafiti mbalimbali za nchi zilizoendelea zimebainisha kuwa vuimbe hai vinavyoishi sehemu hizo vipo kwenye hatari zaidi ya kupata dozi kubwa ya mionzi hiyo. Mwili wa bianadamu wenyewe unauwezo wa kutoa dozi ya chini sana ya mionzi kama 10hertz, na kila chembechembe ya mwili wetu ina mionzi yake ( cellular electromagnetic field) ,Watafiti wamesema  frequency za kutengenezwa zinazozidi 10 hertz zinaweza sababisha  msongo wa mawazo, matatizo ya kukosa usingizi, matatizo ya kizazi na saratani mbailimbali endapo binadamu atapata dozi hiyo kwa muda mrefu.

Minara ya simu ina mionzi yenye nguvu zaidi kulinganisha na mionzi ya radio (the higher the frequency the more powerful the wave = more powerful effects on biological organisms) na kumbuka mionzi ya minara ya simu ina nguvu 1900 MHz. Mionzi hii inauwezo waa kuharibu bond ya molekula na chemicali na kusababisha mabadiliko ya vinasaba (DNA), Metabilism,vichocheo vya mwili (hormones) na enzyemes hali inayopelekea madhara yafuatayo ya kiafya:

                        1. Kuumwa kichwa(headache)
                        2.  Kukosa kumbukumbu(memory loss)
                        3. Kupungua kwa mbegu za kiume za uzazi (low sperm count)
                        4.  Saratani na kasoro za uzazi
                        5.  Matatizo ya moyo
                        6.  Msongo wa mawazo
                        7. Kukosa usingizi.

Kibaya zaidi mionzi hii ina tabia ya kujilimbikiza kwenye mwili (body accumulation) na kuja kuonesha madhara miaka kadhaa inayofuata kutegemea na mtu na mtu na hali ya afya ya mtu.
Chanzo:  mtandao  wa   ujenzionline
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright Daniel Blog in Contemporary News
Back To Top