WANAUME wanaotumia muda wa saa tatu na zaidi kwa siku kutazama
runinga wanapoteza nguvu za kiume ukilinganisha na wale wanaotazama
runinga mara chache.Utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Afya ya
Umma cha Havard (HSPH) kilichopo Boston nchini Marekani, umebaini kuwa
kuporomoka kwa kiwango cha mbegu za kiume kunahusiana moja kwa moja na
kutofanya mazoezi na kutazama runinga kwa muda mrefu.
Imeelezwa kuwa wanaume wanaotazama runinga kwa
zaidi ya saa 20 kila wiki wanapoteza asilimia 44 ya mbegu za kiume
ukilinganisha na wale wasiotumia muda mrefu katika runinga.Vilevile, wanaume wanaofanya mazoezi kwa zaidi
ya saa 15 kwa wiki, wana uwezo wa kuongeza asilimia 73 ya mbegu zao
ukilinganisha na wale wasiofanya mazoezi au wanaofanya mazoezi chini ya
saa tano kwa wiki.
Kiongozi wa utafiti huo, Dk Audrey Gaskin
alisema mtindo wa maisha unachochea zaidi upungufu wa mbegu za kiume na
uzalishwaji wa mbegu za kiume.Mtafiti huyo alifanya uchunguzi wa viwango vya
mbegu za kiume za wanaume 189 wenye umri wa kati ya miaka 18 na 22
kuanzia mwaka 2009 hadi 2010.
Soma zaidi : http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1687952/-/11sd59u/-/index.html
Soma zaidi : http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1687952/-/11sd59u/-/index.html
Post a Comment