Social Icons

Loading...

Utalii wa ngono waingia nchini.

KATIKA hali ya kawaida, tumezoea kuona watalii kutoka mataifa mbalimbali duniani wakija nchini kuangalia vivutio vya utalii vilivyopo.Baadhi ya vivutio hivi ni Mlima Kilimanjaro, mbuga za wanyama, majengo ya kale, mapango na nyumba za kihistoria.Hata hivyo, kumeibuka aina mpya ya utalii, unaojulikana kama utalii wa ngono, ambao unashamiri kwa kasi ukihusisha zaidi watalii wanawake wanaofuata wanaume wa Kitanzania hasa vijana.
        Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi Jumapili, unaonyesha kuwa utalii huo unaongezeka kwa kasi hasa katika maeneo yenye vivutio vingi vya utalii ikiwamo Arusha, Kilimanjaro na Zanzibar.
Imebainika kuwa katika utalii huu, wanawake hasa watu wazima walio na umri kati ya miaka 60 hadi 80 kutoka nchi mbalimbali, wamekuwa wakiingia nchini kwa lengo la kutafuta vijana wa kiume wa kustarehe nao.Uchunguzi huo unaonyesha kuwa wanawake ambao hawana vigezo vya uzuri vinavyopendwa na wanaume huko kwao, ikiwamo wembamba na urefu, husafiri kuja Tanzania kutafuta mwanamume atakayestarehe naye kingono.Hali hiyo inawakumba zaidi wanawake wanene, ambao kwa Ulaya hukosa wapenzi, hivyo kulazimika kusafiri kuja Afrika Tanzania ikiwamo kutafuta mwenza wa kustarehe nao.
Chanzo: http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1689836/-/11sei33/-/index.html
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright Daniel Blog in Contemporary News
Back To Top