MBUNGE wa Ubungo Jijini Dar es Salaam (Chadema), John Mnyika
amemtaka, Rais Jakaya Kikwete kutosaini marekebisho ya sheria mpya ya
mabadiliko katika Sheria ya Ukaguzi wa Hesabu za Umma ya 2008.Mnyika pia anakusudia kukata rufaa juu ya uamuzi
wa Spika wa Bunge, Anne Makinda kwa kutumia vibaya kanuni za Bunge
kutokana na kitendo chake cha kuzivunja kamati tatu za Hesabu za
Mashirika ya Umma (POAC), Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) na Hesabu
za Serikali Kuu (PAC).
Akizungumza na Mwananchi Jumapili, jana, Mnyika
alisema Rais Kikwete kabla ya kusaini marekebisho hayo ambayo
yanaonyesha dalili za kuwalinda mafisadi, ajitokeze na kuwaeleza
Watanzania faida na hasara ya mabadiliko ya sheria hiyo.
Wiki hii Serikali iliwasilisha bungeni mapendekezo
ya mabadiliko katika Sheria ya Ukaguzi wa Hesabu za Umma ya 2008, huku
ikiongeza vifungu ambavyo vinapunguza nguvu ya Bunge katika
kushughulikia taarifa ya Ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za
Serikali (CAG).
Soma zaidi : http://www.mwananchi.co.tz/habari/-/1597578/1689870/-/vlipm8/-/index.html
Soma zaidi : http://www.mwananchi.co.tz/habari/-/1597578/1689870/-/vlipm8/-/index.html
Post a Comment