Mwenyekiti
wa Kamati ya Mambo yaNje na Ushirikiano wa Kimataifa, Edward Lowassa,
amemtahadhalisha kujiepusha na kauli za kuunga mkono ushoga.
Lowassa
ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, ameliambia NIPASHE Jumapili ofisini
kwake jijini hapa jana kuwa ushoga na hai za ndoa kwa watu wa jinsia
moja vinaweza `kuiharibu’ ziara yake hapa nchini.
Mapema
wiki hii, Rais Obama alikaririwa akizungumzia masuala hayo yanayotajwa
kuwa ni moja ya haki za msingi za binadamu, alipokuwa Senegal, lakini
akapingwa.
“Watanzania
hawatalikubali na wataendelea kushikilia uhuru na heshima
walizojengewa tangu awali, kwamba ushoga na ndoa za jinsia moja
havikubaliki,” alisema.
Akiwa Senegal, Rais Obama alitaka serikali za Afrika kutoa haki kwa mashoga kama inavyotoa kwa raia wengine.
"Ninachotegemea,
I pray and hope (ninasali na kutegemea) kwamba kuhusu mashoga na ndoa
za jinsia moja, Rais Obama hatarudia kauli aliyoitoa kule Senegal,” alisema.
Aliongeza,
"ninasema hivi kwa sababu Tanzania hatuamini katika ushoga, na endapo
utawalazimisha Watanzania, watakukatalia na kushikilia uhuru na heshima
waliyojengewa toka awali."
AHIMIZA MAPOKEZI MAZURI
Hata hivyo, Lowassa aliwataka Watanzania kuiheshimu na kuitumiavema
fursa ya kutembelewa na Rais Obama, hivyo wajitokeze kumlaki kwa wingi.
"Tutambue
mataifa makubwa yanakimbilia maslahi ya karne inayofuata, kwa mfano
Rais wa China, Xi Jiping siku moja baada ya kuapishwa kwake alikuja
hapa nchini, " alisema.
Hivyo,
alitoa wito kwa Watanzania kuhakikisha maslahi na fursa za kiuchumi
zinakuwa za kwanza kulindwa, kwa kuwa ziara hiyo itafungua milango
zaidi kwa wawekezaji kuja nchini.
Pia,
Lowassa alisema ziara ya Rais Obama ni kielelezo cha amani na usalama
uliopo, na kwamba itasaidia kuwavutia watalii na wadau wa sekta
nyingine za maendeleo kuitembelea Tanzania.
KITUO CHA KIJESHI
Kuhusu hofu na tetesi kuwa ziara hiyo imelenga taifa hilo kuja hapa
nchini kufungua kituo cha kujiimarisha kiulinzi, Lowassa alisema
Watanzania wanapaswa kufahamu kuwa tayari nchi hiyo ina kituo cha
kijeshi nchini Kenya.
"Tuangalie
maslahi yetu tuachane na mitazamo hasi, kama ni kituo cha kijeshi
tayari kipo Kenya, tujiulize kwa nini marais wa Marekani Bill Clinton
na George Bush walivyofanyaziara zao hapa nchini hawakwenda Kenya,"
alisema.
WALINZI WA NDANI KUWEKWA KANDO
Kuhusu ziara hiyo kutumia ulinzi wa kimataifa huku majeshi ya Tanzania
yakiwekwa kando kwa ushiriki wa moja kwa moja, Lowassa alisema Rais wa
Marekani ana kiwango cha juu cha ulinzi unaosimamiwa na nchiyake pekee.
"Ni
sahihi walinzi wetu kukaa pembeni, huyu ni kama Rais wa dunia, lakini
hata majeshi yetu yanafanya kazi ya ulinzi lakini sio kwamba yatakaa
nyuma tu," alisema.
SUMAYE: TUMKARIBISHE
Naye, Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick
Sumaye, alisema ziara ya Rais Obama haina ujumbe zaidi ya kuhimiza watu
wajitokeze kumpokea.
Hata
hivyo, Sumaye alikwepa kuzungumzia kwa undani hatua ya kuwafukuza
wafanyabiashara kutoka kandoni mwa barabara, ili kupisha mapokezi ya
Rais Obama.
“Ninachokielewa
ni kuwa barabara ambazo wanapita viongozi kama Rais Obama zinatakiwa
kuwa katikahali ya usalama na hivyo kutakiwa kuboreshwa,” alisema.
LIPUMBA: MAFANIKIO NI MADOGO KIUCHUMI
Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba, alisema
mafanikio ya ziaraya Rais Obama yapo katika kujitangaza kimataifa
kuliko kiuchumi.
Profesa
Lipumba ambaye ni mchumi aliyebobea, alisema changamoto iliyopo ni
kwamba bado biashara kati ya nchi mbili hizo siyo kubwa kama ilivyo kwa
nchi kama China na Tanzania.
Alitolea
mfano, mwaka 2012 bidhaa za hapa nchini zilizouzwa Marekani zilikuwa
na thamani ya Dola milioni 66 ikilinganishwa na zile zilizouzwa China
ambapo zilikuwa ni zaidi ya Dola milioni 500.
Alisema
bidhaa zilizoagizwa kutoka Marekani zilikuwa na thamani ya Dola
milioni 230 huku za kutoka China zikiwa na thamani ya zaidi ya Dola
milioni 1,100.
"Utakubaliana
nami kuwa mahusiano yetu na China ni makubwa kuliko Marekani licha ya
nchi hii kutoa fursa kwetu ambazo hatujazitumia ipasavyo," alisema
Profesa
Lipumba alisema Marekani kupitia mpango wake wa kusaidia Maendeleo ya
Afrika (AGOA), ulitoa fursa kwa bidhaa za Afrika kuuzwa nchini humo
bila ushuru, lakini Tanzania haikuitumia.
Pia
alisema utawala wa George Bush, uliisaidia Tanzania kupitia Mfuko wa
Changamoto za Milenia (Millenium Challenge Compact (MCC) kupewa Dola
milioni 700 kwa ajili ya kusaidia miundombinu na ujenzi wa nyaya za
umeme kutoka bandarini hadi Zanzibar.
"Pana
uwezekano wa mpango wa pili wa MCC, Tanzania ikapata msaada wa
kuimarisha miundombinu ya umeme, lakini pia kampuni za Marekani kuja
kuwekeza hapa kwetu," alisema.
Alisema
uwekezaji wa kampuni hizoutategemeana na wafanyabiashara wa hapa nchini
pamoja na serikali kutumia fursa mbalimbali za nchi hiyo.
Katika
hatua nyingine, Profesa Lipumba alisema ili nchi iweze kujikwamua na
umasikini itatokana na jinsi itakavyotumia sera na juhudina siyo
kutegemea msaada kutoka nje.
HOTELI ZIMEJAA
Wingi wa wageni wakiwamo
watakaofika kwa ajili ya ziara ya Rais Obama, umesababisha hoteli
nyingi za jijini Dar es Salaam `kujaa’.
Uchunguzi
wa NIPASHE Jumapili ulibaini kwamba kwa zaidi ya wiki sasa, hoteli
nyingi hazikupokea wageni kutokana na kile kilichoelezwa kuwa, nyingine
zililipiwa ingawa vyumba havikutumika kwa wakati.
POLISI: WASIO NA KAZI WASIJE MJINI
Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga,
amewataka wananchi ambao hawatakuwa na mambo muhimu ya kufanya katikati
ya jiji, wasifike huko kupunguza msongamano wa watu na magari baada ya
kuwasili kwa Rais Obama.
Alisema, baadhi ya barabara zitafungwa kwa muda kwa ajili ya viongozi kuzitumia, hivyo kusababisha msongamano.
Hekaheka zimetanda jijini Dar es Salaam, ikiwa ni zaidi ya saa 24 kabla ya kuwasili kwa Rais Barack Obama.
Rais
Obama, atawasili nchini kesho akitokea Afrika Kusini, ambapo pamoja na
mambo mengine, alizungumza katika mkutano wa ‘viongozi vijana wa
Afrika’ na kujibu maswali kutoka nchi tofauti.
Mkutano
huo ulifanyika jana jioni huko Soweto nchini Afrika Kusini, ambapo
alipokewaa na kujibu maswali kutoka Kenya, Uganda, Nigeria na Afrika
Kusini kwenyewe.
Jijini
Dar es Salaam, shughuli kadhaazikiwamo za ulinzi na usalama,
zinafanyika kwa kasi na umakini kuhakikisha ziara ya Rais Obama
inafanyika pasipo bughudha. kujibu maswali kutoka Kenya, Uganda, Nigeria
na Afrika Kusini kwenyewe.
Jijini
Dar es Salaam, shughuli kadhaazikiwamo za ulinzi na usalama,
zinafanyika kwa kasi na umakini kuhakikisha ziara ya Rais Obama
inafanyika pasipo bughudha.
Hata
hivyo, sehemu kubwa inayohusu masuala ya itifaki, ulinzi na usalama
yanafanywa na taasisi za Marekani, kwa kuzishirikisha taasisi za ndani
kwa kiwango kidogo.
“Hawa
jamaa (Wamarekani) wanapoingia nchi yeyote wakiwa naRais wao, shughuli
nyingi na uamuzi wanafanya wao, sisi wa ndani inakuwa kushirikishwa
kwa kiasi kidogo,” kilieleza chanzo cha NIPASHE Jumapili kutoka moja ya
taasisi zinahusika katika ziara hiyo.
Maeneo
kadhaa ya jijini humo, yaliendelea kudhibitiwa kwa ulinzi mkali na
doria za mara kwa mara, huku kandoni mwa baadhi ya barabara wakionekana
askari wa Jeshi la Wananchi (JWTZ).
Mathalani, kandoni mwa barabara ya Morogoro, eneo la Ubungo, walionekana askari wa JWTZ maarufu kama MP.
Shughuli
nyingine zimehusisha pia operesheni zinazofanywa na polisi kwa
kusaidiana na mgambo wa jiji, kuhakikisha watu na bidhaa zilizopokandoni
mwa barabara zitakazotumika kwa ziara ya Rais Obama, vinaondolewa.
Magari
yaliyowabeba polisi wenye silaha za moto na mabomu ya machozi,
yalionekana katika mitaa kadhaa jijini humu, wakihakikisha operesheni
hiyo inafanyika pasipo kikwazo kutoka kwa wahusika.
Kila
palipofanyika operesheni hiyo, baadhi ya askari walifanya doria zamu
kwa zamu, kuhakikisha kuwa bidhaa na watu walioondolewa, hawarejei.
Hata
hivyo, waathirika katika operesheni hiyo walieleza kutofurahia, huku
wakihoji ni kwa nini serikali haikuwaandalia mazingira mbadala kabla ya
utekelezaji wake.
Walisema
miongoni mwao, wamekopa mitaji kutoka kwenye taasisi za kifedha, hivyo
kusimamisha biashara zao ili kupisha ujio wa Rais Obama, kutawaweka
katika hali ngumu kiuchumi.
“Ikiwa
ujio wa Rais Obama unatutesa wafanyabiashara kiasi hiki, ni vigumu
kuhimili maisha yetu, kwa sababu hatujui hatma yetu baada ya yeye
kuondoka,” alisema mfanyabiashara Zena Rashidi wa Kariakoo.
Hata hivyo, wamachinga walionekana jana katika kituo cha mabasi cha Mwenge walipofukuzwa, wakiwa wanaendelea na biashara zao.
Lakini
walifanya hivyo kwa tahadhali ikiwamo kushika bidhaa chache mikononi,
huku wakitumia 'janja' ya kupiga kelele za 'kumsifia' Rais Obama.
Walisikika
miongoni mwao wakisema, 'praise to Obama' na wengine wakaitikia
'aaamen'. Walifanya hivyo zamu kwa zamu, lakini haikujulisha
waliashiria nini.
BARABARA ZAPAMBWA
Aidha, barabara zote atakazopita Obama wakati wa ziara yake zimepambwa
kwa bendera za Marekani na Tanzania; huku zikinakshiwa kwa picha yake
ambayo imeandikwa 'President Barack Obama' karibu Tanzania.
Barabara
hizo ni ile ya Nyerere kuanzia uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu
Julius K. Nyerere, Ali Hassan Mwinyi, Mwai Kibaki na Bagamoyo.
NIPASHE
Jumapili imeshuhudia pichana bendera hizo zikiwa zimewekwa kwenye
mabango yote yaliyo barabarani kuanzia Ikulu hadi kwenye barabara hizo
huku usafi wa jiji ukionekana kuimarika zaidi. Jana
gazeti hili lilishuhudia karibu barabara zote, vijana wanaofanyakazi
ya kuweka bendera na picha ya Obama wakifanyakazi hiyo. CHANZO: NIPASHE JUMAPILI