Kampuni ya Ndege ya Fly540 imesaini makubaliano na Shirika la
Ndege la Qatar Airways, yenye lengo la kuwezesha abiria wa Qatar Airways
kuendelea na safari za ndani na kanda kwa kutumia ndege za Fly540.
Chini ya makubaliano hayo, abiria wa Qatar Airways
baada ya kufika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, Kenya,
wataendelea na safari zao mbalimbali kwa kutumia ndege za Fly540.
Shirika hilo la Ndege la Qatar huruka mara mbili
kwa siku kwenye safari ya Nairobi-Doha, wasafiri wanaweza kuunga safari
nyingine katika miji mikubwa barani Ulaya, Mashariki ya Kati na Asia
Pacific.
Qatar Airways ilisema uamuzi wake wa kuchagua
Fly540 kuwa kama mbia, unadhihirisha dhamira ya shirika hilo lenye
makazi yake Doha kufanya uwekezaji eneo la Afrika Mashariki.
Msemaji wa Shirika la Fly540 la Kenya, alisema
makubaliano hayo yanadhirisha jinsi shirika hilo linavyoaminika na
kuhudumia mashirika makubwa kama la Qatar Airways.
“Tunayo furaha kufikia makubaliano haya na Shirika
la Ndege la Qatar, ambayo ni makubaliano yetu ya kwanza ya pekee,”
alisema Ofisa Mtendaji Mkuu wa Fly540 Kenya, Don Smith. Safari hizo
zinahusisha Zanzibar, Juba na vivutio vya utalii.
Post a Comment