Waziri
wa Mambo ya Nje, Bernard Membe amewashauri watu walioko mikoani
kusitisha safari za kuja Dar es Salaam wakati wa ziara ya Rais wa
Marekani, Barrack Obama kutokana na wingi wa wageni katika jiji hilo.
Ugeni huo pamoja na ule wa viongozi
kumi na moja kutoka nchi mbalimbali duniani watakaohudhuria mkutano wa
kimataifa wa Smart Partnership utakaofunguliwa kesho na Rais Jakaya
Kikwete kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere,
umesababisha kuimarishwa kwa ulinzi katika maeneo mbalimbali hasa katika
hoteli za kitalii ambazo zimeanza utaratibu wa upekuzi kwa wageni wake.Akizungumza na katika mahojiano na Redio ya Clouds jana, Membe alisema jiji limefurika kwa wingi wa wageni.
“Hoteli na nyumba za wageni zimefurika
wageni na magari mengi yamekodiwa. Kwa ujumla, huduma za kijamii
zitakuwa shida,” alisema.
Rais Obama na mkewe Michelle watawasili
nchini Jumatatu na tayari wapambe na maofisa usalama kutokana Marekani
wameanza kuwasili. Mbali ya ujio huo, wake wa marais kutoka nchi 14 za
Afrika watakaokutana na Laura Bush, mke wa Rais wa zamani wa Marekani,
George Bush. Pia Michelle atahudhuria mkutano huo utakaofanyika Jumanne
na Jumatano ijayo.
“Jiji la Dar es Salaam litakuwa na mambo mengi kwa hiyo wale wenye kuja kutaka kustarehe wafute safari zao,”alisema na kuongeza: “Kama
kuna watu ambao hawapo Dar es Salaam na hawana sababu za kuja mjini
waache tu mpaka wageni watakapoondoka kwa sababu jiji la litakuwa
limejaa na baadhi ya barabara zitachukuliwa zitumike na wageni hao.”
Alisema katika kipindi cha siku tano
zijazo, baadhi ya barabara za Jiji la Dar es Salaam zitakuwa na shughuli
nyingi na nyingine zitalazimika kufungwa. Barabara itakayofungwa ni
pamoja na ile ya Mwai Kibaki na ile ya Bagamoyo itakuwa na shughuli
nyingi pia wakati Michelle atakapokwenda Jumba la Makumbusho, Jumanne
ijayo.
Wasafiri wa mikoani
Wasafiri wa mikoani wataathirika zaidi
Jumanne ijayo wakati Rais Obama atakapokwenda kutembelea mitambo ya
kufua umeme ya Kampuni ya Symbion Ubungo.
Kituo hicho kipo Barabara ya Morogoro, ambayo ndiyo inayotumiwa na magari yanayoingia na kutoka mikoani.
Rais Obama atakwenda katika kituo hicho
yapata saa 4.00 asubuhi na kwa kiasi kikubwa itaathiri magari ya
usafirishaji wa mizigo na abiria yatakayokuwa yanatoka na kuingia Dar es
Salaam kabla na wakati huo.
Post a Comment