Social Icons

Loading...

ARUSHA KWACHAFUKA .

Jeshi la polisi limekipiga marufuku chama cha demokrasia na maendelo(CHADEMA)kufanya shughuli zozote za kuaga miili ya marehemu kwenye viwanja vya Soweto kwani zoezi la uchunguzi bado linaendelea kwenye viwanja hivyo huku mabomu yakirindima uwanjani hapo.

Akizungumza ofisini kwake kamanda wa polisi mkoani hapa Liberatus Sabas alisema kutokana na uchunguzi unaoendelea wa tukio la bomu kwenye viwanja hivyo imeonelea kuwa si busara kuweka mkusanyiko wa watu kwani kutaharibu upelelezi.
 
Kamanda Sabas alisema kuwa kwa hiyo jeshi hilo limewataka viongozi wa chama hicho kuwaeleza wafuasi wao mahali sahihi watakapoweza kufanyia shughuli hiyo lakini si kwenye viwanja hivyo.

Hali kwenye viwanja hivyo imekuwa ya pilika pilika tangia juzi kwa wafuasi wa chama hicho kujikusanya tokea asubuhi hadi jioni kwa madai ya kuomboleza tukio la bomu la kurushwa kwa mkono lililotokea uwanjani hapo juzi.

Hata hivyo viongozi wa chama cha demokrasia na maendeleo walikuwa wamukusanyana kwenye uwanja huo hali iliyoendelea kuleta mvutano kati ya viongozi  wa jeshi la polisi na  wafuasi hao baada ya kukaidi amri ya jeshi hilo mabomu yalirindima uwanjani hapo.

author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright Daniel Blog in Contemporary News
Back To Top