Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini iliwaona wana kesi ya
kujibu katika mashtaka yote matano yanayowakabili. Katika moja ya
mashtaka hayo, Sheikh Ponda na wenzake anadaiwa kula njama na wizi wa
mali yenye thamani ya Sh59.6 milioni.Awali, Hakimu Mkazi, Victoria Nongwa alitoa
uamuzi kuwa kina Sheikh Ponda wana kesi ya kujibu baada ya kupitia
ushahidi uliotolewa na mashahidi 17 wa upande wa mashtaka, ikaonekana
shauri hilo limetokana na kipande cha ardhi.Kesi hiyo iliposikilizwa mara ya mwisho,
Hakimu Nongwa alisema kuwa baada ya Baraza la Waislamu Tanzania
(Bakwata) kubadilisha ardhi ya ekari nne iliyopo Chang’ombe Markazi na
ekari 40 za Kampuni ya Agritanza Ltd zilizopo Kisarawe, kuna baadhi ya
Waislamu hawakuridhika.
Mbali na mashtaka hayo, Ponda na mshitakiwa
mwingine Sheikh Mukadam Abdallah Swalehe wanakabiliwa na shtaka la
uchochezi wakidaiwa kuwa kati ya Oktoba 12 na 16, mwaka jana katika eneo
la Chang’ombe Markazi, wakiwa viongozi wa Taasisi na Jumuiya za
Kiislamu Tanzania, waliwashawishi wafuasi wao kutenda makosa hayo.
Chanzo mwananchi.
Chanzo mwananchi.
Post a Comment