Amani ya kutoka kwa Mungu haitokani na mazingira tunayopitia au mambo
tunayokutana nayo. Amani ya Mungu huja kwetu na kudumu bila kujali
tunapitia hali gani. Amani hii inatokana na kuwa na uhusiano mzuri na
Mungu, kitambua kuwa siku zetu zipo mikononi mwa Mungu, na kufahamu kuwa
Mungu ndiye mpaji wa vitu vyote. Amani hii ni matokeo ya moyo uliotulia
mbele za ungu.
Haimaanishi kuwa hakuna matatizo, ila amani ya kristo inakuwepo pale
unapoamini kuwa Mungu yupo katikati yako hata unapopita katika matatizo.
Ni lazima uwe na imani timilifu kwa Mungu, na kumtegemea yeye pekee.
Isaya 26:3 Utamlimda yeye ambaye moyo wake umekutegemea Katika amani kamilifu kwa kuwa anakutumaini.
Pia unapolifuata neno la Mungu utapata amani ya kweli.
Zaburi 119:165 Wana amani nyingi waipendao sheria yako, Wala hawana la kuwakwaza.
Neno la Mungu linaondoa hofu na wasiwasi na kukupa amani ndani ya moyo wako. Roho mtakatifu hutufariji na kutupa amani katika magumu tunayoyapitia.
Unapokutana na jambo linalokukosesha amani, kwanza omba kwa Mungu
akujalie amani yake ipitayo akili zote. Tambua ukuu wa Mungu, uwezo
wake, upendo na uaminifu wake. Yeye anauwezo wa kukupa amani ya kweli
siku zote na katika hali zote.Pia unapolifuata neno la Mungu utapata amani ya kweli.

Post a Comment