Mvua zinazoendelea kunyesha Dar es Salaam hasa maeneo ya kati kati ya jiji , asubuhi hii hali ilikuwa hivi...
Asubuhi hii barabarani viatu vilipumzika kidogo na kisha suruali kukunjwa hadi magotini ili kuweza kuvuka na kuelekea ofisini, hali ilikuwa mbaya.
Boda Boda nazo mwendo mdundo.
Huyu ni ofisa wa benki maarufu katika mtaa huu akivuka kueleka ofisini kwake .
Kufa kufaana , kuna vijana wa MUJINI nao walikuwa kama kawaida kutengeza dili za kuvusha watu , ukiwa Posta kijana huyo ni nadra sana kumkosa hasa katika dili zake za kuwahi siti katika daladala zinazoelekea Mwenge au Mbagala kwa Tsh 500, leo asubuhi dili lilibadirika ghafla ikawa ni kuvusha abiria kwa kuwabeba , Hapa ni kama anamwambia MREMBO huyo anayepita " karibu upande mgongoni nikuvushe" mrembo naye wala haoneshi kushawishika! KAZI NI KAZI.
Rami ikiwa imefunikwa na maji .

5 comments
duuh...hi kali
ReplyHii sasa ni Kero! Du!
ReplyPoleni sana wana Dar Es Salaam! Inabidi serikali ianze mikakati yakuboresha mifereji ili mvua kama hizi zisizuie au kufanya usafiri kua kero kwani sasa maji taka na yamvua si yanaweza kusababisha magonjwa jamani!
ReplyTunashukuru kwa kutujuza
ReplyDuh karne hii bado hizi sehemu zinafurika baada ya mvua ya 2 hrs. Vipi ikinyesha 12 hrs ??
ReplyPost a Comment