Social Icons

Loading...

Hali si shwari Simba Sports Club … Hans Pope na Kaburu Wajiuzulu

ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Zacharia Hans Poppe,  ameamua kujiuzulu nyadhifa zote hizo kwa sababu kuna mgawanyiko ndani ya uongozi unaokwamisha maendeleo.
“Ni wazi kuwa kwenye uongozi tumekuwa hatufanyi kazi kwa umoja na mgawanyiko huu unatukwaza na hatuwezi kupata maendeleo,”alisema Hans Poppe.
“Baada ya kutafakari, nimeona ni bora nijiuzulu nyadhifa hizo kupisha wengine ambao wanaweza wakawa na mawazo mapya ya kuendeleza klabu, nami nitabakia kuwa mwanachama mwaminifu daima,”alisema Hans Poppe.
Poppe amewasilisha barua ya kujiuzulu Simba SC  jana na wazi kujiuzulu kwa Kapteni huyo wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) ni pigo kwa klabu hiyo, kwani alikuwa akiisaidia mno kwa hali na mali.Aidha, kujiuzulu kwa Hans Poppe wazi kutachochea zaidi mgogoro ndani ya klabu hiyo na kuongeza shinikizo la viongozi wa klabu hiyo kujiuzulu pia.
Simba SC kwa sasa haifanyi vizuri katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na tayari imekwishatolewa katika Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kufungwa jumla ya mabao 5-0 na Recreativo de Libolo ya Angola katika raundi ya kwanza tu.
Ubingwa wa Ligi Kuu ni kama umekwishaota mbawa, kwani hadi sasa Wekundu hao wa Msimbazi wanashika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 31, sawa na Coastal Union ya Tanga na Mtibwa Sugar ya Morogoro, nyuma ya Azam FC yenye pointi 36 na Yanga inayoongoza kwa pointi zake 42, zote za Dar es Salaam.
Godfrey Nyange naye ajiuzulu kwa e-mail
MAKAMU Mwenyekiti wa Simba SC, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ inadaiwa amemuandikia barua pepe, Mwenyekiti wa klabu hiyo, Alhaj Ismail Aden Rage kumtaarifu kujiuzulu wadhifa huo.Kaburu anakuwa kiongozi wa pili wa Kamati ya Utendaji ya Simba kujiuzulu , baada ya awali mchana, Zacharia Hans Poppe aliyekuwa Mjumbe kujiuzulu pia.
Hans Poppe, aliyekuwa pia Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, alisema kwamba ameamua kujiuzulu nyadhifa zote hizo kwa sababu kuna mgawanyiko ndani ya uongozi unaokwamisha maendeleo.
Chanzo :  Bin  Zubeiry  Blog.
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright Daniel Blog in Contemporary News
Back To Top