MZUNGUKO wa pili ya Ligi Kuu ya Vodacom utaanza Januari 26
mwaka huu huku kukiwa na maombi ya televisheni ya SuperSport kuonyesha mechi za
Super Week kama ilivyokuwa katika mzunguko wa kwanza.
Raundi tano za awali katika ratiba ya mzunguko wa pili
zinabaki kama zilivyo wakati nyingine zilizobaki zitatolewa baada ya kuingiza
mechi za Super Week.
Wakati huo huo, mzunguko wa pili wa Ligi Daraja la Kwanza
unatarajia kuanza Januari 26 mwaka huu. Ratiba ya ligi hiyo na tarehe rasmi ya
kuanza itatangazwa baada ya kupitiwa na Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Mpira
wa Miguu Tanzania (TFF) inayotarajiwa kukutana mwishoni mwa wiki.
This post was written by: Author Name
Your description comes here!
Get Free Email Updates to your Inbox!
on Thursday, January 17, 2013
Post a Comment