Social Icons

Loading...

Kampuni ya Tigo yagoma kupunguza gharama za simu.

WAKATI Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikiwasilisha rai ya kupunguza gharama za mwingiliano wa simu , Kampuni ya Tigo imekataa kufanya hivyo kwa madai kuwa itahatarisha uwekezaji wake kwa punguzo la asilimia 69.
Msimamo huo wa Tigo, umekuja baada ya TCRA kukutana na wadau wa mawasiliano jana jijini Dar es salaam, ili kukusanya maoni kuhusu mapendekezo ya kupunguza gharama ya mtandao mmoja kwenda mwingine. Hatua hiyo inalenga katika kuwasaidia wananchi kumudu gharama za mawasiliano ya simu.Naibu Mkurugenzi wa Utekelezaji wa Kanda wa TCRA, Victor Nkya, alisema punguzo hilo ni la kutoka asilimia 35 hadi asilimia 69 na kwamba litaanza kutumika Machi mosi mwaka huu na kukoma Desemba 31 mwaka 2017 .
Nkya alisema punguzo la gharama ya kupiga mtandao mmoja kwenda mwingine kwa mwaka 2013 litakuwa asilimia 34.92, mwaka 2014 asilimia 32.40, mwaka 2015 asilimia 30.18, mwaka 2016 asilimia 28.57 na mwaka 2017 ni asilimia 26.96.
Zaidi  Fuatilia  hapa  : http://www.mwananchi.co.tz/-/1597570/1668454/-/xkrt34/-/index.html
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright Daniel Blog in Contemporary News
Back To Top