Social Icons

Loading...

Marufuku wanawake kukaa kiume kwenye pikipiki

Jiji moja nchini Indonesia ambalo limekuwa likifuata sheria za kiislamu maarufu kama sharia, liko mbioni kupitisha sheria ya kuwapiga marufuku wanawake kukaa kiume kwenye pikipiki, zenye kuendeshwa na wanaume, kwa madai kuwa mkao huo huwaondolea uthamani wao
Suaidi Yahya, ambaye ni meya wa jiji hilo la Lhokseumawe, ameeleza kuwa, mpango huo umelenga katika kutunza mila na desturi za watu na tayari vipeperushi kwa ajili ya kusambaza taarifa juu ya kusudio la mpango huo, vimeshaanza kusambazwa mitaani.
      Chini ya sheria mpya, meya huyo anasema kuwa, wanawake wataruhusiwa tu kupanda pikipiki wakiwa wamekaa kiupande upande (kike), kwakuwa kukaa kiume ni ukiukwaji wa sheria za kiislamu.
“Ukimuona mwanamke amekaa kiume kwenye pikipiki, anaonekana kama mwanaume tu, lakini akikaa kike, anaonekana kama mwanamke kweli” amesema meya huyo na kuongeza pia kuwa, watu wenye kupanda pikipiki na kukaa mkao wa kike, pia hawapati ajali za kuanguka kwa urahisi.
Mamlaka za mji huo, zinatarajiwa kuanza kufanya mapitio ya muswada huo katika muda wa mwezi mmoja na ikiwa wataridhia basi utapitishwa na kuwa sheria ndogo ya jiji hilo.
     Alipoulizwa ikiwa wanawake ambao hawatatimiza sharti hilo watachukuliwa hatua, meya huyo alijibu “ndio, mara tu itakapopitishwa na kuwa sheria rasmi, hakika kutakuwa na adhabu itayotolewa”
Hata hivyo, muswada huu, umekutana na vipingamizi toka kwa watu mbalimbali akiwemo mwanaharakati wa masuala ya kiislamu, Ulil Abshar Abdalla, mwenye makazi yake kwenye mji mkuu wa Indonesia wa Jakarta.
“Uendeshaji au upakiaji wa pikipiki haujawekewa kanuni katika quran tukufu wala kwenye hadith za kiislamu ambazo ndio chimbuko la maelekezo yetu” amesema mwanaharakati huyo
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright Daniel Blog in Contemporary News
Back To Top