Social Icons

Loading...

Obama Aapishwa Rasmi.

RAIS Barack Obama wa Marekani ameapishwa rasmi kushika muhula wa pili wa urais, katika sherehe maalumu iliyofanyika kwenye Ikulu ya nchi hiyo jana.
Obama ambaye ni Rais wa 44 wa Marekani, aliingia madarakani katika uchaguzi wa kihistoria mwaka 2008 uliomfanya kuwa Rais wa kwanza mwenye asili ya Afrika katika taifa hilo kubwa duniani.Sherehe za kuapishwa kwake Ikulu jana zilikuwa za faragha na zilihudhuriwa na watu wachache maalumu, leo ataapishwa katika sherehe za jumla zitakazowajumuisha watu wote kwenye Uwanja wa National Mall.
Katika kiapo chake, Obama atatumia Biblia mbili, moja iliyokuwa ikitumiwa na Martin Luther King na nyingine ilikuwa ikitumiwa na aliyekuwa Rais wa 16 wa Marekani, Abraham Lincoln.
      Lincoln aliongoza taifa hilo kuanzia Machi 1861 hadi alipouawa Aprili 1865.
Akiwa Ikulu jana, alitumia Biblia iliyowahi kutumiwa na Lincoln, katika sherehe za leo  atatumia Biblia ya Martin Luther King.Lincoln, ndiye aliyeliongoza taifa hilo kipindi kigumu cha kusimamia umoja na kufuta biashara ya utumwa.Martin Luther King ambaye alikuwa mchungaji na mwanaharakati wa haki za watu wenye asili ya Afrika nchini Marekani, aliuawa Aprili 4, 1968, muda mfupi baada ya kutoa hotuba yenye nguvu ya I have a Dream (Nimeota ndoto).Hotuba hiyo ikuwa ikieleza ndoto yake kwamba muda siyo mrefu watu wenye asili ya Afrika watapata nguvu na kupata haki yao kama raia wa Marekani.
Soma  zaidi : http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kimataifa/-/1597284/1671080/-/14b41t5z/-/index.html
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright Daniel Blog in Contemporary News
Back To Top