SAKATA la kupinga ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara kwenda 
Dar es Salaam limechukua sura mpya baada ya wananchi zaidi ya 30,000 
kusaini katika fomu maalumu kupinga gesi hiyo kusafirishwa.Wakati wananchi hao wakikamilisha shughuli hiyo na
 kukabidhi fomu hizo kwa wabunge wa Chama cha Wananchi (CUF), umoja wa 
vyama tisa vya siasa mkoani umemwomba Rais Jakaya Kikwete kusitisha 
mradi huo ili kuepusha uvunjifu wa amani unaoweza kujitokeza.Pia, 
umoja huo umewataka wabunge wote wa Mkoa wa Mtwara kutangaza msimamo wa 
kila mmoja juu ya gesi kwenda Dar es Salaam au kukubaliana na uamuzi wa 
Serikali ili wajue nani msaliti kwao.
        Wakizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika
 jana katika Uwanja wa Sabasaba mjini hapa, viongozi hao kwa nyakati 
tofauti wamemtaka Rais Kikwete kutokutumia ‘jazba na mabavu’ katika 
kulipatia suluhu jambo hilo, badala yake busara zitawale kwa kusitisha 
mradi huo.“Sisi Watanzania hatujazoea vita, bali tumezoea kupata 
hasara… katika hili naomba Kikwete akubali kupata hasara kama 
tunavyokubali hasara nyingine…Sisi wananchi tupo radhi tuingie kwenye 
deni kubwa kama hilo, lakini gesi haiwezi kwenda Dar es Salaam,” alisema
 Uledi Abdallah Makamu, Mwenyekiti wa umoja huo na kuongeza:“Hizo trilioni tatu kama anaona hawezi kuzilipa 
iwapo gesi itabakia Mtwara...Basi atafute njia nyingine za kulipa… 
Atambue kuwa hakuna fedha yenye thamani ya amani na utulivu 
wetu…akumbuke kuwa mafahali wawili hawakai zizi moja.”Naye Mwenyekiti wa
 Chadema Wilaya ya Mtwara Mjini, Mustafa Nchia aliwataka wabunge kutoa 
misimamo yao ili wananchi wajue ni mbunge yupi anawaunga mkono na yupi 
msaliti kwao.
Soma Zaidi : http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1671038/-/11rm8cs/-/index.html
Soma Zaidi : http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1671038/-/11rm8cs/-/index.html





Post a Comment