WABUNGE vijana katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
wameanza kujiandikisha tayari kwa kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa
(JKT) kwa Mujibu wa Sheria kwa ajili ya mafunzo yatakayoanza Machi mwaka
huu.Taarifa ambazo Mwananchi Jumamosi ilizipata juzi,
zimeeleza kuwa, idadi ya wabunge ambao tayari wamejiandikisha kujiunga
na JKT hadi sasa ni zaidi ya 31, huku wengine wakiendelea.
Kujiandikisha kwa wabunge hao ili wajiunge na JKT
kunafuatia wito uliotolewa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga
Taifa, Shamsi Vuai Nahodha, Julai mwaka uliopita, alipowasilisha hotuba
ya bajeti ya wizara yake katika Bunge la Bajeti mjini Dodoma.
Kwa nyakati tofauti wabunge vijana kutoka CCM,
Chadema na NCCR- Mageuzi walilithibitishia gazeti hili kuwa tayari
wamejiandikisha katika Ofisi ya Katibu wa Bunge kwa ajili ya mafunzo
hayo.Imebainishwa kuwa, miongoni mwa wabunge
waliojiandikisha, wamo pia ambao waliwahi kupitia mafunzo hayo,
ikielezwa kuwa wamefanya hivyo wakitaka kwenda kujikumbushia.
Soma Zaidi : http://www.mwananchi.co.tz/habari/Siasa/-/1597332/1669540/-/bolrnxz/-/index.html
Soma Zaidi : http://www.mwananchi.co.tz/habari/Siasa/-/1597332/1669540/-/bolrnxz/-/index.html
Post a Comment