Social Icons

Loading...

DIGITAL CAMERA INATAFUTWA


  KUNA  MDAU  ANATAKA  KUNUNUA  DIGITAL  CAMERA  YA  UKWELI,  KAMA  WEWE  NI  MUUZAJI  AU  UNAUZA  YA  KWAKO   IWE  MPYA
SPECIFICATION:
1. IWE  AINA  YA  SONY  AU  SUM SUNG
2. IWE  NA  MEGA PIXEL  KUANZIA   16  NA  KUENDELEA

Kwa  mawasiliano   tumia  simu 
+255715058970  au  mail   netnewstz@gmail.com

UEFA Super Cup 2012: Falcao, Atletico Run Wild Over Chelsea 4-1

The 2012 edition of the UEFA Super Cup, pitting the current Champions League holder Chelsea against the current Europa League holder Atletico Madrid was indeed super...in an incredibly lopsided way.

                               Radamel  Falcao  scores 3 goals  -  The  man of  the  Match.



Chelsea looked listless and disinterested, and Atletico took advantage riding a Falcao hat trick to a 4-1 thrashing of the Blues.



Zoezi la uokoaji Kivuko cha Mv Magogoni lafana ..

Wiki hii  Jeshi  la  wananchi  la  Tanzania  kikosi cha   wanamaji      linaendesha    zoezi/ Onesho  la  namna  ya  kupambana    na  majanga  ya  ajali  za  majini katika  Kivuko  cha  Kigamboni, ikiwa  ni   sehemu  ya  maadhimisho  ya  siku  ya  majeshi nchini   1  September .
         Waathirika  wa  ajali  wakiwa  kati  kati  ya  mkondo  wa  bahari  , wakisubiri  kuokolewa
                          Mfano  wa  ajali  ya  majini,   waathirika  wakitapatapa  kuhitaji  msaada  wa  uokozi.

                                Boti  ya  jeshi  ikielekea  sehemu  ya  tukio  tayari  kwa  uokozi.
                                                         Feri  -  Kigamboni

                        Boti  ikiwa  inaondoka  eneo la  tukio   baada  ya   uokoaji  kukamilika.

Mdau Emmanuel Mniko apata Mtoto wa Pili.

Tunamshukuru  Mwenyezi  Mungu  kwa  baraka   alizowajalia    Familia   ya  Mr  & Mrs  Mniko   a.k.a  Mchwali ,   mdau  huyo   amewahi  kufanya  kazi kwa nyakati  tofauti  UCC  tawi  la  Mwanza,  Plan International   Geita,   SITA  Group  of  companies  Dar es  Salaam   kisha akaamua  kutimukia     jiji la Adelaide, South Australia   ambako  ndiko  anaishi  kwa sasa yeye   pamoja  na  familia  yake.-   HONGERENI  SANA.
                                       Mdau   Mniko  akiwa  amempakata  mtoto  Selisha

M4C kama Airtel Vile........


John Lisu Kuwasha Moto CCC Jumapili ya tarehe 2 Sept, 2012


Twite Ataweza kukidhi kiu na hamasa hii ya Wana Yanga??

TWITE, Twite, Twite' kiitikio 'Rage, Rage, Rage' ndiyo wimbo  uliotawala jana kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wakati beki mpya wa Yanga, Mbuyu Twite alipowasili akitokea Rwanda.
Wimbo huo ulikuwa ukiimbwa na mamia ya mashabiki wa Yanga wake kwa waume waliofurika uwanjani hapo kwa ajili ya kumpokea beki huyo.

Kwa wiki kadhaa Twite aliteka hisia za mashabiki wa timu za Yanga na Simba ambazo ni baada ya beki huyo kusajiliwa na timu hizo kabla ya yeye mwenyewe kuikana Simba na kuamua kuichezea Yanga.Kitendo hicho, kilisababisha kuzuka kwa malumbano baina ya viongozi wa klabu hizo mbili na kufuatiwa na tamko la Makamu mwenyekiti wa Simba, Godfrey Nyange Kaburu kusema kuwa watamkamata Twite na kumfikisha kwenye vyombo vya sheria  atakapokanyaga ardhi ya Tanzania.

Hata hivyo licha ya vitisho hivyo vya Kaburu, hakuna kiongozi yeyote wa Simba aliyeonekana uwanjani hapo kumsubiri beki huyo kwa ajili ya kumtia mikononi kama ilivyotarajiwa.

Mara baada ya kuwasili uwanjani hapo majira ya saa10.30 jioni, Twite alipokewa na viongozi wa Yanga wakiongozwa na katibu mkuu wa timu hiyo, Selestine Mwesigwa na alikabidhiwa jezi namba 4 yenye jina la Rage  kama ushindi dhidi ya wapinzani wao Simba.

Mara baada ya kukabidhiwa jezi hiyo, Twite alizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa umati aliouhushuhudia uwanjani hapo ulimpa moyo wa kuona jinsi mashabiki wa Yanga wanavyomjali.

"Nimeshangaa sana kuona watu wengi kiasi hiki, hii inadhihirisha ni kiasi gani mashabiki wananijali, nami nasema sitawaangusha, jambo la muhimu ni ushirikiano tu kutoka kwao na uongozi mzima wa Yanga ili malengo yafikiwe,"alisema Twite.Alipoulizwa anazungumziaje mpango wa Simba kutaka kumkamata kwa madai ya kuwatapeli, Twite alisema,"kwa sasa siwezi kuzungumzia hilo, nadhani nitafanya hivyo baadaye."

Baada ya mahojiano na Wanahabari, Twite alipanda gari dogo na moja kwa moja msafara ulioongozwa na mabasi yaliyokuwa yamebeba mashabiki wa Yanga ulielekea makao makuu ya klabu hiyo yaliyoko Mtaa wa Jangwani.

Wafanya uharibifu mkubwa

Tukio jingine lililojiri uwanjani hapo ni lile la mashabiki kuharibu mandhari nzuri ya eneo la maegesho ya uwanja huo wa ndege kwa kukanyaga maua ili kutaka kumuona Twite aliyekuwa akilindwa na makomandoo wa Yanga.

Njiani
Wakati msafara wa Yanga ulipokuwa ukipita barabara ya Nyerere kuelekea Jangani, mashabiki wa Yanga waliokuwa wakitembea kwa mguu walikuwa wakiwashangilia huku wale wa Simba walikuwa wakionyesha vidole vitano juu kumaanisha mabao 5-0 waliowafunga Yanga katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu uliopita.
Taarifa  kwa  hisani  ya  http://www.mwananchi.co.tz/michezo/-/25885-twite-twite-rage-rage

Changamkia nafasi hii kama una kipaji ...


Kibonzo


Mhe Hawa Ngulume Afariki

Bi Hawa Ngulume, aliyewahi kuwa Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Bagamoyo na Mbarali, amefariki dunia jijini Dar es Salaam leo asubuhi. Mama Ngulume amekuwa akisumbuliwa na maradhi ya kansa kwa kipindi kirefu na mauti yamemfika akiwa katika hospitali ya Lugalo jijini Dar.Kwa kujibu wa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana taratibu za mazishi zinaandaliwa na taarifa kamili itatolewa hapo baadaye.
Source : Radio  One  Breaking  News Alert.

Taarifa kwa Umma kuhusu Mauaji ya Morogoro

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinapinga kauli za Serikali, Jeshi la Polisi na Chama Cha Mapinduzi (CCM) zenye kulipotosha taifa kuhusu mashambulizi na mauji yanayoelezwa kufanywa na askari Mkoani Morogoro na badala yake kinataka uchunguzi huru ufanyike haraka kwa mujibu wa Sheria ya Uchunguzi wa Vifo (Inquest Act).

Kauli zilizotolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani zina mwelekeo wa kulilinda Jeshi la Polisi ambalo askari na maofisa wake ni sehemu ya watuhumiwa wa mauaji, badala ya kuwezesha ukweli kuthibitika na hatua kuchukuliwa kwa wahusika.

Hivyokutokana na kujirudiarudia kwa mauaji yanayofanywa na vyombo vya dola CHADEMA kinatoa mwito kwa Rais Jakaya Kikwete ambaye kwa mujibu wa katiba ibara ya 33 ni mkuu wa nchi, kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu aingilie na kuwezesha uchunguzi wa kina.

Ikumbukwe kwamba tarehe 27 Agosti 2012 Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro lilifyatua risasi za moto na kupiga mabomu ya machozi wananchi na wanachama wa CHADEMA waliokuwa wamejikusanya kwa ajili ya kuelekea kwenye mkutano halali wa CHADEMA na wengine waliokuwa wakiendelea na shughuli zao eneo la Msamvu, hivyo kusababisha kifo cha raia mmoja asiye na hatia na kujeruhi wengine wawili.

CHADEMA kinaukumbusha umma kwamba kwa mauaji hayo na mengine katika maeneo mbalimbali nchini serikali inayoongozwa na CCM kupitia vyombo vya dola inaendelea kukiuka Ibara ya 14 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo inatambua kwamba uhai ni haki ya msingi kwa raia wote.

CHADEMA hakikubaliani na hatua zilizochukuliwa na Serikali mpaka sasa kuhusu tukio husika pamoja na maelezo yaliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani tarehe 28 Agosti 2012 ambayo kwa sehemu kubwa yametokana na taarifa zisizo za kweli kutoka kwa maofisa wa Jeshi la Polisi ambao ni sehemu ya watuhumiwa wa mauaji husika.

CHADEMA haina imani na timu iliyoundwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi kuchunguza tuhuma za askari kufyatua risasi na mabomu ya machozi na kusababisha mauaji kwa kuwa tayari serikali na Jeshi la Polisi wametoa maelezo yenye kutofautiana kwa kiwango kikubwa na maelezo ya mashuhuda waliokuwepo na ushahidi wa picha za eneo la tukio.

Wakati Serikali na Jeshi la Polisi wakitoa maelezo kuwa marehemu alikutwa umbali wa mita 300 na kupelekwa hospitali na wasamaria wema, mashuhuda wameeleza wazi kuwa askari walifika jirani na eneo lake na ofisa mmoja akaonyesha ishara na ndipo risasi za moto na mabomu ya machozi yakafyatuliwa mojawapo kumpata marehemu na kudondoka.

Mashuhuda wote waliohojiwa wanaeleza kwamba bunduki ya polisi ndiyo ilielekezwa na kufyatuliwa kwa marehemu, maelezo pekee yanayotofautiana ni kuwa baadhi wameeleza kuwa ni bunduki ya risasi za moto na wengine wa wameeleza kuwa ni bunduki ya kufyatulia mabomu ya machozi.

Mara baada ya kudondoka gari hilo liliondoka na gari lingine la polisi lilifika likiongozwa na Kamanda wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia cha Mkoa ambaye alitoa amri ya gari lingine kumbeba Ali Hassan Singano (Zona) na kuondoka naye, hivyo si kweli kwamba matukio hayo yalitokea mbali na eneo bali pembeni ya meza ya muuza magazeti huyo karibu na barabara ya kwenda Iringa eneo ambalo polisi ilikuwa ikifanya mashambulizi.

Kauli zilizotolewa na Serikali kuwa Jeshi la Polisi lilizuia maandamano ya CHADEMA yaliyopangwa kufanyika Mkoani Morogoro kwa sababu ya sensa ya watu na makazi si za kweli kwa kuwa sababu pekee zilizotolewa ni ufinyu wa barabara na kuwa maandamano yalipangwa siku ya kazi. Ushahidi wa suala hili ni barua ya Jeshi la Polisi lenyewe ya 23 Agosti 2012 yenye Kumb. Na. MOR/A.25/1/VOL. II/202.

CHADEMA kinaujulisha umma kwamba Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro ndilo lililoacha kuheshimu utawala wa sheria na makubaliano yaliyofikiwa baada ya mazungumzo yaliyohusisha kikosi kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi kikiongozwa na Kamanda wa Operesheni za Jeshi hilo Simon Siro na hivyo kuwa chanzo cha mauaji yaliyotokea na madhara mengine kwa wananchi waliokuwepo maeneo yaliyorushiwa mabomu ya machozi.

Ikumbukwe kwamba awali CHADEMA kilipanga kufanya maandamano na mikutano katika Jimbo la Morogoro Mjini tarehe 4 Agosti 2012 na kuwasilisha taarifa kwa Jeshi la Polisi kwa mujibu wa sheria.
Hata hivyo, Polisi wakakataa kufanyika kwa maandamano na mikutano kwa kisingizio cha Sikukuu ya Nanenane, mgomo wa walimu na ratiba kugongana na ile ya mikutano ya CCM, sababu ambazo zilibainika kwamba hazikuwa na msingi wowote.

Baada ya mvutano na mazungumzo CHADEMA ilikubali kutii sheria na kuzingatia matakwa ya Jeshi la Polisi pamoja na kuwa yalitolewa kinyume cha Sheria kwamba maandamano na mkutano wa CHADEMA vifanyike mara baada ya siku ya kuanza kwa sensa tarehe 26 Agosti 2012 na CHADEMA ilipendekeza tarehe 27 Agosti 2012 ambayo Jeshi la Polisi liliikubali.

Polisi walifanya hivyo wakielewa ukubwa wa barabara za Morogoro na pia wakitambua kwamba ilikuwa ni siku ya kazi, hata hivyo tarehe 23 Agosti 2012 Jeshi la Polisi liliandika barua ya kueleza kwamba limetoa kibali cha mkutano (suala ambalo si mamlaka yake kisheria) na pia limekataza maandamano.

CHADEMA kikaamua kwa mara nyingine tena kurudi katika meza ya mazungumzo na Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro, tarehe 24 Agosti 2012 ambapo polisi ilikubali maandamano ikiwemo ya watembea kwa miguu na kupendekeza njia mbadala na tarehe 26 Agosti 2012 mazungumzo yakaendelea kwa lengo la kukagua barabara.

Hata hivyo, kufuatia shinikizo la Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro Faustine Shilogile kinyume na Sheria ya Jeshi la Polisi ambayo imetoa mamlaka kwa Mkuu wa Polisi Wilaya kuhusu taarifa za mikutano, polisi ikarejea katika msimamo wa kukataza mapokezi ya watembea kwa miguu na badala yake tarehe 26 Agosti 2012 bila sababu za misingi ya kisheria na zisizozingatia haki za kikatiba ikapendekeza kwamba yafanyike mapokezi kwa kutumia magari.

Maelezo ya Waziri wa Mambo ya Ndani kuwa iwapo vyama vya siasa visiporidhika na mazingira kama hayo yapo mamlaka ya kukata rufaa yanapotosha kwa kuwa Sheria ya Jeshi la Polisi na Sheria ya Vyama vya Siasa hazijaweka utaratibu wa rufaa hivyo njia pekee ya kisheria ni kutumia mahakama.

Jeshi la Polisi lingeheshimu utawala wa sheria na mazungumzo lingeruhusu CHADEMA ifanye maandamano na kutoa ulinzi mpaka eneo la mkutano kwa muda mfupi badala yake jeshi hilo likaamua kutumia nguvu kubwa na kusababisha mauaji, barabara kufungwa kwa muda mrefu na kuathiri wananchi waliokuwa wakiendelea na kazi zao.

Iwapo wanachama na wananchi waliokuwa wamekusanyika kuwapokea viongozi na kuelekea kwenye mkutano wangekuwa wamekiuka sheria Jeshi la Polisi lingeweza kuwakamata kwa mujibu wa sheria, hata hivyo hakuna kiongozi yoyote wa CHADEMA aliyefunguliwa jalada mpaka sasa katika kituo chochote cha polisi kwa kudaiwa kukiuka sheria.

Kinyume chake Jeshi la Polisi ambalo likiwa kwenye mazungumzo lilikubali kuwa mapokezi yafanyike kwa msafara wa vyombo vya moto, lakini tarehe 27 Agosti 2012 likaamua kupiga mabomu ya machozi kwa wananchi na wanachama wa CHADEMA waliokuwa wamekusanyika eneo la Msamvu wakiwasubiri viongozi bila hata ya kusubiri kuona iwapo yangefanyika matembezi ya miguu kuelekea eneo la mkutano au maandamano ya magari na vyombo vingine vya usafiri.

Kitendo cha Jeshi la Polisi kutumia nguvu kubwa kinyume cha sheria na kusababisha mauaji na kufunga barabara kwa muda mrefu kiliwafanya wanachama wa CHADEMA na wananchi kwa ujumla kutawanyika kuelekea eneo la mkutano na wengine kuingia barabarani kutembea kuelekea eneo la mkutano na hatimaye polisi walipoona wamesababisha hali hiyo wakaamua kulinda misafara hiyo mpaka eneo la mkutano hali inayodhihirisha kuwa uamuzi kama huo ungechukuliwa kutoka mwanzo yasingetokea madhara yoyote.

Kwa kuzingatia utofauti mkubwa baina ya maelezo yanayotolewa na Serikali na Jeshi la Polisi kuhusu matukio husika na ukweli halisi ulivyotokea, CHADEMA kinasisitiza kuwauchunguzi huru ufanyike kwa mujibu wa Sheria ya Uchunguzi wa Vifo (Inquest Act) Sura ya 24 ya Sheria za Tanzania.

CHADEMA kwa mara nyingine kinaitaka Serikali inayoongozwa na CCM kurejea katika kifungu cha 3 cha Sheria ya Uchunguzi wa Vifo, ambacho kinatoa mamlaka ya Waziri mwenye dhamana na masuala ya Sheria kuanzisha Mahakama ya Kuchunguza Vifo hivyo (Coroner’s Court) katika maeneo ya serikali za mitaa kwa kushirikiana na Jaji Kiongozi.

CHADEMA kinaikumbusha Serikali kuwa, kufuatia kauli ya Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Mawaziri Vivuli husika kueleza bungeni taarifa za mauaji yaliyofanywa na vyombo vya dola kwa nyakati mbalimbali, Waziri Mkuu na Mawaziri wengine waliahidi bungeni kwamba sheria hiyo itaanza kutumika kuchunguza vifo vyenye utata.

Katika muktadha huo uchunguzi wa kifo cha Ali Zona haupaswi kufanywa na timu ya polisi bali sheria hiyo sasa ianze kutumika.

Kwa upande mwingine, CHADEMA imeheshimu taratibu za maziko zilizopangwa na familia ambapo mwili wa marehemu ulisafirishwa jana tarehe 28 Agosti 2012 kwenda Mkoani Tanga kwa ajili ya maziko na CHADEMA kuwasilisha rambirambi zake za awali, taarifa zaidi kuhusu ushiriki kwa CHADEMA kwenye maziko zitaelezwa baada ya majadiliano yanayoendelea na familia.

CHADEMA kwa kuheshimu mazungumzo na utawala wa sheria kwa mara nyingine tena tarehe 28 Agosti 2012 CHADEMA kimesitisha Operesheni za Maandamano na Mikutano yake ya Vuguvugu la Mabadiliko (M4C) kwa rai iliyotolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) ili kupisha kukamilika kwa zoezi la sensa ambayo imetokana pia na maelezo ya mamlaka zingine za kiserikali.

CHADEMA inatambua kwamba wakati maandamano ya CHADEMA yametolewa rai kuwa yasitishwe kupisha sensa, maandamano ya wagombea wa CCM kurudisha fomu za uchaguzi wa ndani ya chama chao yameachwa yakiendelea katika barabara kadhaa nchini bila kusitishwa kwa kisingizio hicho.

Aidha, wakati CHADEMA ikiheshimu mazungumzo na kusogeza ratiba yake mbele ya tarehe 26 Agosti 2012 mpaka tarehe 27 Agosti 2012 kupisha sensa hatua ambayo ilifanywa pia na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, ambayo ilitangaza ratiba yake kuendelea baaada ya tarehe hiyo.

Tume hiyo inaendelea na mikutano yake ya hadhara inayokutanisha wananchi katika kata za mikoa mbalimbali wakati huo huo zoezi la sensa likiendelea lakini kwa mikutano ya CHADEMA inaonekana kufanyika kwake ni kuingilia sensa.

CHADEMA inataka Serikali na Polisi kueleza iwapo matukio haya na mengine hayana mwelekeo wa ubaguzi na uhujumu wa vuguvuvugu la mabadiliko linaloendelea nchini kwa kurejea ukweli kuwa maisha ya wachache yanaweza kuwekwa mashakani lakini si mabadiliko kwa maslahi ya wengi.

CHADEMA itaeleza hatua za ziada itakazochukua baada ya kupata ripoti ya uchunguzi wa mwili wa marehemu (post mortem) uliofanyika tarehe 28 Agosti 2012 na uamuzi wa Serikali kukubali au kukataa mwito wa kutumia Sheria ya Uchunguzi wa Vifo (Inquest Act) kuwezesha uchunguzi huru.

Imetolewa tarehe 29 Agosti 2012 na:
John Mnyika (Mb)
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi

Real Madrid 2 Barca 1 Yatwaa Super Cup


Hatimaye    Madrid yafuta  uteja  dhidi   ya  Barca  Yatwaa      La  Liga - SUPA  CUP


 







  

KIU Ya http://www.facebook.com/ Mpaka ICU


Waliogoma Kuhesabiwa Washikiliwa na Jeshi la Polisi - Mbeya


Licha ya Rais Jakaya Kikwete kuwataka waislamu  nchini kushiriki zoezi la Sensa  ya watu makazi, hali hiyo imeonekana kuwa tatizo kwa kijiji cha Ruiwa Kata ya Ruiwa Wilayani Mbarali  ambapo watu wasita wanaosadikiwa kuwa ni waislamu  wenye msimamo mkali kugoma kuhesabiwa  kwa madai  kuwa serikali imepuuza  madai yao.

Imeelezwa kuwa waislamu hao walishaeleza serikali kuwa hawako tayari kuhesabiswa lakini bado serikali imeshindwa kutekeleza matakwa yao na hivyo kukataa kuhesabiwa.

Akizungumza na gazeti hili jana kuhusiana na madai hayo , Ofisa Mtendaji wa Kata ya Ruiwa Bw. Jordan Masweve alisema kuwa kwa kata zoezi la sense toka limeanza imekuwa ni tatizo kubwa sana kutokana na watu hao kuonyesha msimamo wao wa kutotaka kuhesabiwa.

“Wao wanadai kuwa hawapo tayari kuhesabiwa hata iweje msimamo wao ni mmoja hata wafanywe nini lakini suala ni kutokubali kuhesabiwa tu kwa madai serikali imeepuza madai yao toka mwanzo ya kutotaka kuhesabiwa”alisema.

Bw. Masweve alisema tukio hilo limetokea  Agosti 27 mwaka huu majira ya saa 8.30 mchana  katika kijiji cha Ruiwa wakati makarani wa sense  walipofika katika makazi wa wananchi hao  wakiongozwa na Mtendaji wa kijiji  kwa lengo la kuwataka wakubali kuhesabiwa lakini waligoma.

Alisema  hata hivyo zilifanyika jitiha za kuwasihi kushiriki zoezi hilo  lakini hawakutaka kukubali  ndipo mgambo wa kijiji walipowakamata na kuwapeleka kwenye ofisi ya Kata.

Bw. Masweve aliwataja waislamu waliokamatwa kuwa ni Ally Mwangoto,Subeti Juma, Abinala, Pembe ,Ally Suleiman pamoja na Nawab Suleiman licha ya kufikishwa katika ofisi ya kata bado waliendelea kuwa na msimamo wao  kuwa hawako tayari kuhesabiwa na kudai kuwa vyovyote itakavyokuwea wapo tayari  hata kuchinjwa au kufungwa jela lakini si kuhesabiwa.

Hata hivyo alisema kuwa waislamu hao walidai kuwa hata Mkuu wa Wilaya akifika hapo hawako tayari kuhesabiwa msimamo wao ni mmoja tu .

“Bado tupo nao hapa ofisini tukisubiri Mkuu wa Wilaya ya Mbarali ,na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Mbarali ili waje kuwachukua  watu hawa”alisema.

Aidha aliongeza kuwa kabla ya zoezi hilo kuanza  kulikuwa na mikutano ya  hadhara ambayo ulikuwa unaendeshwa na  viongozi wa kiislamu kutoka Jijini Mbeya  walikuwa wakihamasisha waislamu wenzao kuwa ambao hawatakuwa tayari kushiriki zoezi hilo kukimbilia misikitini ambako watawapelekea chakula mpaka zoezi hilo litakapokuwa limekamilika.

Akizungumza kwa njia ya simu akiwa njiani kuelekea kijiji cha Ruiwa  Mkuu wa Wilaya Mbarali Bw. Gulamu Hussen Kiffu alisema amepata taarifa za tukio hilo lakini bado hajafika huko lakini yupo njiani kuelekea huko ili aweze kujua undani wa tukio hilo.

“Kwasasa nipo kwenye gari naelekea Ruiwa kwa ajili ya tukio hilo mara baada ya kufika na kuangalia tukio lilivyo nitatoa taarifa kamili na hatua zipi ambazo tutakuwa tumechukua”alisema.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Bw.Athuman Diwani alisema bado hajapata taarifa hizo na kudai kuwa taarifa zote za matokeo atatotoa mara baada ya zoezi la sense kumalizika.
Picha na Habari na Ezekiel Kamanga,Mbarali 

Likizo : Drogba Afanya Mazoezi na Chelsea

Mtandao wa Give me football umeripoti kwamba Mkali wa soka Didier Drogba ambae baada ya mkataba wake na Chelsea kuisha alisaini dili jipya na club ya Shenhua ya China, amerudi na kuonekana kwenye mazoezi na Chelsea.
Katika kipindi hiki cha mapumziko kwenye msimu wa soka China, Drogba amerudi London kuisalimia familia yake lakini pia alionekana kwenye uwanja wa mazoezi na Chelsea.
Give me Football wamezidi kutiririka kwamba kuna uwezekano huo ndio ukawa mwisho wa Drogba kuichezea Shenhua baada ya kugundulika kwamba club hiyo inahangaika kutafuta pesa za kuendelea kuwalipa wachezaji wake kutokana na pesa nyingi kutolewa kwa mishahara ya Drogba na Anelka.
Kutokana na club hiyo kuwa na tatizo la kifedha kwa sasa upo uwezekano mkubwa wa Drogba na Anelka kuuzwa kwenye club nyingine ili angalau hizo pesa zisaidie kuiokoa Shenhua, kutokana na hilo pia kwa sasa kuna uwezekano mkubwa wa Drogba kurudi kuichezea Chelsea kama itakubali kuilipa Shenhua.
picha  na  taarifa    kwa  hisani ya http://millardayo.com/taarifa-kamili-kuhusu-didier-drogba-kuonekana-tena-chelsea/  

Kibonzo, Adha za Daladala....


Tawi Jipya la Chadema Houston Nchini Marekani lafunguliwa

Baada ya kufungua Tawi jijini Washington DC tarehe 27 MAY 2012, Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimefungua tawi lingine la pili tarehe 25 AUGUST 2012 jijini Houston, Texas nchini Marekani ikiwa ni muendelezo wa kufungua matawi mbalimbali nchini humo. 

Mwenyekiti wa Chadema Taifa Mhe Freeman Mbowe akizungumza muda mfupi baada ya kuzindua tawi jipya la Chadema Houston,Tx nchini Marekani

Sherehe hiyo ya Ufunguzi wa Tawi la Chadema Houston imehudhuriwa na Mwenyekiti wa Chadema Taifa Mhe Freeman Mbowe na Mbunge wa Mbeya mjini Mhe Joseph Mbilinyi "Sugu". Viongozi wengine waliohudhuria ni Katibu wa Chadema Tawi la Washington DC Mhe Isidory Lyamuya na aliyekuwa katibu wa Kwanza wa Chadema Washington DC Mhe Liberatus Mwang'ombe. 

Mwenyekiti wa Chadema Taifa Mhe Freeman Mbowe akikabidhi Kadi kwa wanachama wapya wa Chadema nchini Marekani muda mfupi baada ya kuzindua tawi jipya la Chadema Houston
Sherehe hizo ambazo zilifanyika katika Hotel ya Marriot zilihudhuriwa na Watanzania wengi waishio Houston. Katika Sherehe hizo wanachama wengi waliamua kujivua gamba na kuvaa Gwanda kama ishara ya kutaka kulikomboa Taifa la Tanzania linalozama katika Bahari ya Mafisadi. Akiongea katika mkutano huo Mwenyekiti wa Chadema Houston Ndugu Fuefue ameahidi kufanya mambo makubwa kwa kushirikiana na wanachadema wa Houston na wapenda mabadiliko wote kuchangia kwa hali na mali katika operesheni inayoendelea hivi sasa ya M4C. Viongozi hao wa Chadema Houston wameahidi kuchangishana pesa ili kununua gari litakalosaidia katika operesheni ya M4C. Pia wameahidi kutoa pikipiki 116 kama mchango wao kwa Chama kwa ajili ya M4C.
Picha   na  Taarifa  kwa hisani  ya  Mdau    Haki  Ngowi  at  http://www.hakingowi.com
© Copyright Daniel Blog in Contemporary News
Back To Top