Mwenyekiti wa Chadema Taifa Mhe Freeman Mbowe akizungumza
muda mfupi baada ya kuzindua tawi jipya la Chadema Houston,Tx nchini Marekani
Mwenyekiti wa Chadema Taifa Mhe Freeman Mbowe akikabidhi
Kadi kwa wanachama wapya wa Chadema nchini Marekani muda mfupi baada ya
kuzindua tawi jipya la Chadema Houston
|
Sherehe hizo ambazo zilifanyika katika Hotel
ya Marriot zilihudhuriwa na Watanzania wengi waishio Houston. Katika
Sherehe hizo wanachama wengi waliamua kujivua gamba na kuvaa Gwanda kama
ishara ya kutaka kulikomboa Taifa la Tanzania linalozama katika Bahari
ya Mafisadi. Akiongea katika mkutano huo Mwenyekiti wa Chadema Houston
Ndugu Fuefue ameahidi kufanya mambo makubwa kwa kushirikiana na
wanachadema wa Houston na wapenda mabadiliko wote kuchangia kwa hali na
mali katika operesheni inayoendelea hivi sasa ya M4C. Viongozi hao wa
Chadema Houston wameahidi kuchangishana pesa ili kununua gari
litakalosaidia katika operesheni ya M4C. Pia wameahidi kutoa pikipiki
116 kama mchango wao kwa Chama kwa ajili ya M4C.
Picha na Taarifa kwa hisani ya Mdau Haki Ngowi at http://www.hakingowi.com
Post a Comment