Social Icons

Loading...

Twite Ataweza kukidhi kiu na hamasa hii ya Wana Yanga??

TWITE, Twite, Twite' kiitikio 'Rage, Rage, Rage' ndiyo wimbo  uliotawala jana kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wakati beki mpya wa Yanga, Mbuyu Twite alipowasili akitokea Rwanda.
Wimbo huo ulikuwa ukiimbwa na mamia ya mashabiki wa Yanga wake kwa waume waliofurika uwanjani hapo kwa ajili ya kumpokea beki huyo.

Kwa wiki kadhaa Twite aliteka hisia za mashabiki wa timu za Yanga na Simba ambazo ni baada ya beki huyo kusajiliwa na timu hizo kabla ya yeye mwenyewe kuikana Simba na kuamua kuichezea Yanga.Kitendo hicho, kilisababisha kuzuka kwa malumbano baina ya viongozi wa klabu hizo mbili na kufuatiwa na tamko la Makamu mwenyekiti wa Simba, Godfrey Nyange Kaburu kusema kuwa watamkamata Twite na kumfikisha kwenye vyombo vya sheria  atakapokanyaga ardhi ya Tanzania.

Hata hivyo licha ya vitisho hivyo vya Kaburu, hakuna kiongozi yeyote wa Simba aliyeonekana uwanjani hapo kumsubiri beki huyo kwa ajili ya kumtia mikononi kama ilivyotarajiwa.

Mara baada ya kuwasili uwanjani hapo majira ya saa10.30 jioni, Twite alipokewa na viongozi wa Yanga wakiongozwa na katibu mkuu wa timu hiyo, Selestine Mwesigwa na alikabidhiwa jezi namba 4 yenye jina la Rage  kama ushindi dhidi ya wapinzani wao Simba.

Mara baada ya kukabidhiwa jezi hiyo, Twite alizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa umati aliouhushuhudia uwanjani hapo ulimpa moyo wa kuona jinsi mashabiki wa Yanga wanavyomjali.

"Nimeshangaa sana kuona watu wengi kiasi hiki, hii inadhihirisha ni kiasi gani mashabiki wananijali, nami nasema sitawaangusha, jambo la muhimu ni ushirikiano tu kutoka kwao na uongozi mzima wa Yanga ili malengo yafikiwe,"alisema Twite.Alipoulizwa anazungumziaje mpango wa Simba kutaka kumkamata kwa madai ya kuwatapeli, Twite alisema,"kwa sasa siwezi kuzungumzia hilo, nadhani nitafanya hivyo baadaye."

Baada ya mahojiano na Wanahabari, Twite alipanda gari dogo na moja kwa moja msafara ulioongozwa na mabasi yaliyokuwa yamebeba mashabiki wa Yanga ulielekea makao makuu ya klabu hiyo yaliyoko Mtaa wa Jangwani.

Wafanya uharibifu mkubwa

Tukio jingine lililojiri uwanjani hapo ni lile la mashabiki kuharibu mandhari nzuri ya eneo la maegesho ya uwanja huo wa ndege kwa kukanyaga maua ili kutaka kumuona Twite aliyekuwa akilindwa na makomandoo wa Yanga.

Njiani
Wakati msafara wa Yanga ulipokuwa ukipita barabara ya Nyerere kuelekea Jangani, mashabiki wa Yanga waliokuwa wakitembea kwa mguu walikuwa wakiwashangilia huku wale wa Simba walikuwa wakionyesha vidole vitano juu kumaanisha mabao 5-0 waliowafunga Yanga katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu uliopita.
Taarifa  kwa  hisani  ya  http://www.mwananchi.co.tz/michezo/-/25885-twite-twite-rage-rage
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright Daniel Blog in Contemporary News
Back To Top