Licha ya Rais Jakaya Kikwete kuwataka waislamu nchini kushiriki zoezi la Sensa ya watu makazi, hali hiyo imeonekana kuwa tatizo kwa kijiji cha Ruiwa Kata ya Ruiwa Wilayani Mbarali ambapo watu wasita wanaosadikiwa kuwa ni waislamu wenye msimamo mkali kugoma kuhesabiwa kwa madai kuwa serikali imepuuza madai yao.
Imeelezwa
kuwa waislamu hao walishaeleza serikali kuwa hawako tayari kuhesabiswa
lakini bado serikali imeshindwa kutekeleza matakwa yao na hivyo kukataa
kuhesabiwa.
Akizungumza
na gazeti hili jana kuhusiana na madai hayo , Ofisa Mtendaji wa Kata ya
Ruiwa Bw. Jordan Masweve alisema kuwa kwa kata zoezi la sense toka
limeanza imekuwa ni tatizo kubwa sana kutokana na watu hao kuonyesha
msimamo wao wa kutotaka kuhesabiwa.
“Wao
wanadai kuwa hawapo tayari kuhesabiwa hata iweje msimamo wao ni mmoja
hata wafanywe nini lakini suala ni kutokubali kuhesabiwa tu kwa madai
serikali imeepuza madai yao toka mwanzo ya kutotaka kuhesabiwa”alisema.
Bw. Masweve alisema tukio hilo limetokea Agosti 27 mwaka huu majira ya saa 8.30 mchana katika kijiji cha Ruiwa wakati makarani wa sense walipofika katika makazi wa wananchi hao wakiongozwa na Mtendaji wa kijiji kwa lengo la kuwataka wakubali kuhesabiwa lakini waligoma.
Alisema hata hivyo zilifanyika jitiha za kuwasihi kushiriki zoezi hilo lakini hawakutaka kukubali ndipo mgambo wa kijiji walipowakamata na kuwapeleka kwenye ofisi ya Kata.
Bw.
Masweve aliwataja waislamu waliokamatwa kuwa ni Ally Mwangoto,Subeti
Juma, Abinala, Pembe ,Ally Suleiman pamoja na Nawab Suleiman licha ya
kufikishwa katika ofisi ya kata bado waliendelea kuwa na msimamo wao kuwa hawako tayari kuhesabiwa na kudai kuwa vyovyote itakavyokuwea wapo tayari hata kuchinjwa au kufungwa jela lakini si kuhesabiwa.
Hata
hivyo alisema kuwa waislamu hao walidai kuwa hata Mkuu wa Wilaya
akifika hapo hawako tayari kuhesabiwa msimamo wao ni mmoja tu .
“Bado tupo nao hapa ofisini tukisubiri Mkuu wa Wilaya ya Mbarali ,na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Mbarali ili waje kuwachukua watu hawa”alisema.
Aidha aliongeza kuwa kabla ya zoezi hilo kuanza kulikuwa na mikutano ya hadhara ambayo ulikuwa unaendeshwa na viongozi wa kiislamu kutoka Jijini Mbeya walikuwa
wakihamasisha waislamu wenzao kuwa ambao hawatakuwa tayari kushiriki
zoezi hilo kukimbilia misikitini ambako watawapelekea chakula mpaka
zoezi hilo litakapokuwa limekamilika.
Akizungumza kwa njia ya simu akiwa njiani kuelekea kijiji cha Ruiwa Mkuu
wa Wilaya Mbarali Bw. Gulamu Hussen Kiffu alisema amepata taarifa za
tukio hilo lakini bado hajafika huko lakini yupo njiani kuelekea huko
ili aweze kujua undani wa tukio hilo.
“Kwasasa
nipo kwenye gari naelekea Ruiwa kwa ajili ya tukio hilo mara baada ya
kufika na kuangalia tukio lilivyo nitatoa taarifa kamili na hatua zipi
ambazo tutakuwa tumechukua”alisema.
Kwa
upande wake Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Bw.Athuman Diwani alisema
bado hajapata taarifa hizo na kudai kuwa taarifa zote za matokeo
atatotoa mara baada ya zoezi la sense kumalizika.
Picha na Habari na Ezekiel Kamanga,Mbarali
Post a Comment