Ngao ya Hisani iliyotwaliwa na Simba Sports Club kuzindua msimu wa ligi ya 2012/2013 |
Nahodha na golikipa namba moja wa Simba Juma Kaseja akinyanyua juu ngao ya hisani |
Nahodha wa klabu ya Simba Juma Kaseja Juma anapokea ngao ya
hisani kwa mwaka wa pili mfululizo; anapokea ngao ya hisani ya kufungua pazia
la msimu wa mwaka 2012/2013 toka kwa Naibu waziri wa Kazi, vijana na michezo
Mhe. Makongoro Mahanga.
Baada ya Azam kutangulia kwa "baiskeli ya miti" kwa magoli ya
Kipre Tchetche na John Bocco “Adebayor” Simba ilikuja kwa kasi na uzito wa kiberenge na kusawazisha magoli hayo na
kuongeza lingine kupitia kwa Daniel Akuffor (penati), Emmanuel Okwi na Mwinyi
Kazimoto. Simba imeshinda mabao 3 kwa 2 ya Azam FC.
Azam FC wanalia hasa Salum Abubakar kwa kushindwa kutwaa
ngao hii. Shomari Kapombe anaibuka mchezaji bora wa mechi ya leo, ingawa
Emmanuel Okwi na Mrisho Ngasa walimeikimbiza mno ngome ya Azam FC. Pamoja na
ushindi huu kocha wa Simba Mirovan nCircovic ana kibarua kizito kuisuka ngome
yake ya ulinzi kwani bado haijatulia.
Ushindi huu wa pili mfululizo unamaanisha kuwa ikiwa klabu ya Simba itanyakua tena ngao hiyo katika msimu ujao itakuwa imeitwaa ngao hiyo ya hisani jumla/moja kwa moja na hivyo kuandika historia mpya nchini. Simba ndio pia walikuwa wa kwanza kunyakua ngao hiyo tangu mfumo huu ulivyoanza nchini.
Kwa ushindi huu unaifanya klabu ya Simba mpaka sasa kuwa imejikusanyia makombe manne (4) katika mwaka huu wa 2012; makombe mengine ni kombe la ligi kuu ya Tanzania Bara "Vodacom Premier League", Kombe la Urafiki na kombe la mashindano ya muungano.
Pamoja na ushindi huu kocha wa Simba bado ana kibarua kizito kurekebisha mapungufu lukuki katika safu yake ya ulinzi hasa mabeki wa kati na pia kwenye nafasi ya ushambuliaji kwani wachezaji wake wanapoteza nafasi nyingi sana za kufunga magoli.
Post a Comment