Viongozi wa Chama cha walimu wakitangaza msimamo wao kuhusu mgomo wa walimu nchi nzima. |
Chama
cha Walimu Tanzania (CWT) kimetangaza kuanza kwa mgomo wa walimu kwa
nchi nzima kuanzia July 30, mwaka huu baada ya asilimia 95.7 ya walimu
kupiga kura za ndiyo kuridhia kuwepo kwa mgomo huo wa kutetea maslahi
yao.Rais wa CWT Gratian Mkoba amesema kwa mujibu wa sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya mwaka 2004, kifungu cha 80
Moja (d) hatua zote zimefuatwa katika kuandaa mgomo huo na kuwataka
walimu wote washiriki kwa kukaa nyumbani mpaka hapo watakapopewa
maelekezo mengine.Akizungumza
na vyombo vya habari Jijini Dar es Salaam, MUKOBA amesema mgomo huo ni
halali na hauna uhusiano wowote na zoezi la Sensa ya watu na Makazi
linalotarajia kufanyika usiku wa kuamkia tarehe 26, Agosti mwaka huu.
Kuhusiana
na shauri la walimu kuwepo mahakamani Mukoba amesema kitendo hicho
hakiondoi utaratibu wa kuendelea na taratibu za mgomo kutokana na
kutokuwepo kwa amri yoyote ya mahakama kusitisha mgomo huo.
Post a Comment