Wakati mbio za kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu 2015 zikianza
kushika kasi nchini, Rais Jakaya Kikwete amewataka vijana kumchagua mtu
anayefanana na kijana kurithi nafasi yake.
Kauli hiyo ya Rais Kikwete imekuja huku kukiwa na
makada kadhaa ndani ya chama chake ambao wametangaza nia ya kuwania
nafasi hiyo huku baadhi wakifungiwa kwa kuanza kampeni mapema na wengine
wakiendelea na mikakati ya chinichini kabla ya kujitangaza.
Rais Kikwete alisema hayo jana mjini Tabora
alipokuwa akihutubia wananchi waliohudhuria kumbukumbu ya Baba wa Taifa,
Mwalimu Julius Nyerere zilizokwenda sambamba na kilele cha Wiki ya
Vijana na hitimisho la Mbio za Mwenge wa Uhuru.
chanzo : gazeti la mwananchi
chanzo : gazeti la mwananchi
Post a Comment