Kwa wakazi wa Dar es Salaam, moja ya kero kubwa ni kukithiri kwa foleni za magari barabarani.
Hakuna asiyeguswa na atizo hilo kutokana na ubovu wa miundombinu na kutokuwepo na miundombinu ya kisasa ya usafiri ikilinganishwa na ongezeko la watu.
Ni mkoa unaoongoza kwa watu kupoteza muda mwingi
barabarani, kiasi cha kuzorotesha hata utendaji wa kila siku na
kuathiri shughuli za uchumi ambazo ni muhimu kwa maendeleo ya nchi.
Tatizo hili la foleni linaelezewa na wataalamu
kwamba husabisha matatizo mbalimbali ya kiafya, ikiwa ni pamoja na watu
kupatwa na ugonjwa wa kurukwa akili. Kisa cha haya yote ni foleni hizo
ambazo inaonekana wazi kuwa zimekosa mwarobaini wa uhakika.
Hata hivyo, kama sehemu mojawapo ya kukabiliana na
tatizo hilo, Serikali inaendelea na mradi wa mabasi yaendayo kasi.
Kukamilika kwa mradi huo kunaelezwa kuwa kutasaidia kwa kiasi kupunguza
tatizo la foleni barabarani katika baadhi ya maeneo ambayo mradi huo
umeyagusa.
Hata hivyo, baadhi ya wakosoaji wanasema kuwa
kuwapo kwa mradi huo wa mabasi yaendayo kasi hakuwezi kusaidia moja kwa
moja kuondoa tatizo hilo ambalo limeendelea kuongezeka kutokana na
ongezeko kubwa la idadi ya watu na kupanuka kwa shughuli za kiuchumi.
Post a Comment