Social Icons

Loading...

Watatu wakamatwa wakidaiwa kuvuruga Bunge.

Bunge la Katiba jana lilianza kujadili Rasimu ya Katiba kwa misukosuko kwenye Kamati baada ya kuvamiwa na kundi la wanaharakati waliokuwa na mabango wakidai hati halisi ya Muungano yenye saini za Mwalimu Julius Nyerere na Abeid Karume.
Msukosuko mwingine uliozikumba karibu kamati zote zinazoanza kujadili rasimu hiyo kwa kuanzia sura mbili zinazohusu Muungano – sura ya kwanza na ya sita na kuzua malumbano, ni maana ya maneno dola, shirikisho, muungano na nchi.
Wakati waandamanaji wenye mabango wakiishia mikononi mwa polisi, suala la Muungano lilitulizwa kwa kuitwa wanasheria kutoa tafsiri sahihi kwa kila neno.
Katika kamati zote, suala la muda wa kamati kujadili sura hizo mbili kwa siku mbili kila moja pia liliibua mjadala mkali, hadi kuwalazimisha baadhi ya wenyeviti wa kamati kuamua kumwandikia mwenyekiti wa Bunge, Samuel Sitta kuomba muda uongezwe.
Hali hiyo imejitokeza Bunge hilo likiwa limeshakaa siku 40 kabla ya kuingia katika mjadala rasmi, baada ya kupoteza muda mwingi katika kutengeneza kanuni za uendeshaji wa chombo hicho.
http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Watatu-wakamatwa-wakidaiwa-kuvuruga-Bunge/-/1597296/2266274/-/tg1uauz/-/index.html
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright Daniel Blog in Contemporary News
Back To Top