Social Icons

Loading...

BUNGE LA KATIBA LAOMBA KUONGEZEWA SIKU 60

Bunge Maalumu la Katiba limeomba kuongezewa muda wa siku 60 kuanzia Agosti 5, mwaka huu litakapokutana kwa ngwe ya pili.
Bunge hilo linahitimisha ngwe yake ya kwanza Aprili 25, mwaka huu likiwa limekutana kwa siku 67, kati ya 70 zilizokuwa zimetengwa awali.

Kwa muda huo wa ziada 60, iwapo wajumbe wote 629 watalipwa posho ya Sh300,000 iliyopangwa kwa siku, jumla ya Sh11.322 bilioni za walipakodi zitatumika ukilinganisha na Sh13.209 bilioni zilizotumika katika siku 70 za awali. Jumla ya fedha zote zitakazotumika kwa posho ni Sh24.53 bilioni, bila kuingiza gharama nyingine nje ya posho za wajumbe.

Jana, Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta alitangaza kwamba shughuli za Bunge hilo zitakoma wakati wajumbe wake watakapokwenda kusherehekea maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano, Aprili 26, mwaka huu.

Sitta alisema jana kwamba aliwasilisha maombi ya kuongezewa muda kwa Rais Jakaya Kikwete, ambayo yalikuwa hayajajibiwa.

Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue alipoulizwa jana alisema: “Mheshimiwa Rais (Kikwete) anachoafiki ni kama ambavyo kila mtu anaona mwenendo wa Bunge ulivyo, kwamba siku 70 haziwatoshi, hivyo alikubali kwamba wanahitaji kuongezewa muda. Ingawa mpaka sasa hajaamua atawaongezea siku ngapi, atakapoamua tutawafahamisha tu.”

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema alisema upo uwezekano mkubwa wa Bunge hilo kuongezewa siku 60 lakini akaongeza kuwa hilo litategemea bajeti itakayoidhinishwa na Serikali.i 5.
chanzo  fungua  link 
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright Daniel Blog in Contemporary News
Back To Top