Kocha wa Yanga, Hans van Pluijm na mshambuliaji wa Simba, Amis Tambwe kila moja amejigamba kuhakikisha klabu yake inamaliza msimu kwa kupata ushindi katika mchezo wa mwisho baina ya timu hizo.
Kocha huyo Mholanzi ameipongeza Azam kwa kutwaa
ubingwa na kusema waliweka changamoto na presha kubwa hasa katika mechi
zao za mwisho ambazo wote walikuwa wakipambana bega kwa bega kuusaka
ubingwa.
Pluijm alisema anaipongeza Azam kwa kutwaa ubingwa
huo na kudai mechi tatu ziliwaharibia baada ya kutoka katika michuano
ya kimataifa.
“Hatuwezi kulaumiana kwa sasa, tunawapongeza Azam
kwa ubingwa, lakini uzembe wetu umetugharimu kwa kushindwa kutumia
nafasi tuliyokuwa nayo hasa baada ya kutoka katika Ligi ya Mabingwa
Afrika.
“Tulikuwa na michezo mingi mkononi kuliko
wapinzani wetu, lakini tukashindwa kujipanga jambo ambalo lilitugharimu
na kufanya tucheze kwa presha kubwa mechi za mwishoni ili kuusaka
ubingwa, lakini tambua kila timu ilijipanga hivyo tunakubali matokeo,”
alisema.
Pluijm alisema sasa hivi wanaangalia mechi yao ya
mwisho dhidi ya Simba ili waweze kuibuka na ushindi na kujipanga kwa
ajili ya msimu ujao na Kombe la Shirikisho.
“Tuko Moshi leo (jana) tuna mechi ya kirafiki na
baada ya hapo tutarudi Dar es Salaam kuweka kambi kwa ajili ya mechi ya
mwisho ya ligi dhidi ya Simba Jumamosi, naamini tutashinda mechi hiyo
na mambo mengine yatafuata,” alisema Pluijm.
Naye mshambuliaji wa Simba, Tambwe amekiri timu
yao haikuwa vizuri msimu huu, lakini hawatakubali kamwe wafungwe na
Yanga Jumamosi ili kuwafariji mashabiki wao.
Post a Comment