Social Icons

Loading...

KWA HERI WINDOWS XP

Kampuni ya utengenezaji wa mitambo endeshi ya kompyuta (Operating Systems) ya Microsoft ilisitisha utoaji wa huduma za muda mrefu kwa mitambo ya XP, ni moja ya mitambo endeshi inayotumika na watu wengi sana.Tangu kutoka kwa taarifa hizo, kumekuwa na maneno na mikanganyiko mingi mno kwa wateja hususan hapa Tanzania.

Kwakuwa ni mitambo inayotumika kwa weingi kwenye kompyuta nyingi zinazotumika kwenye mabenki na maofisini, hivyo watu walifika mbali hata kusema eti pesa zetu hazipo salama tena. Hivyo, ili kuondoa hofu hizi zinazoizunguka jamii, ungana nasi Dudumizi kwenye kujua nini maana ya kikomo hiki cha huduma na jinsi gani kinaweza kuathiri biashara yako?

 Kwanini XP imefikia kikomo?

XP iliingia sokoni miaka 12 iliyopita, tangu kuingia kwake, imekuwa ni mtambo endeshi unaotumika kwa wingi na makampuni mengi duniani kote. Na pia ni moja ya mtambo endeshi kutoka Microsoft uliokaa kwa muda mrefu sokoni. Ingawa katika uhai wa Windows XP, kumekuwa na matoleo mengine mengi kama Windows Vista, Windows 7 na ya sasa ambayo ni Windows 8, lakini kampuni ya Microfost imeendelea kutoka msaada wa kiufundi na kimatumizi kwa wateja wake wote, hivyo kwa maneno mengine tunaweza kusema,muda wake wa maisha umefika na ni mzigo kiutendaji na hata kibiashara kwa Microsoft kuendelea kuhudumia Windows XP ndiyo maana wameamua kusitisha huduma kwa Windows XP.

Je nini maana ya usisitshwaji wa Huduma?

Hapa ndipo palitokea mkanganyiko miongoni mwa watu wengi, kusitishwa kwa huduma hakumaanishi kuwa kompyuta zote zinazotumia XP hazitotumika tena kama wengine walivyoifananaisha na uhamaji wa mitambo ya analog kwenda Digital. 

Kusitisha kwa huduma kwa XP kunamaanisha, kampuni ya Microfot haitoendelea kutoa huduma (Support) kwa watumiaji wa windows XP tena, huduma hizi ni kama masasisho (updates) ya kiusalama, maboresho ya ufanyaji kazi (kama vile XP SP1, 2..) na huduma nyongine za utumiaji.

Hivyo, unaweza kuendelea kuitumia XP bila shida kama una uhakika kukosa huduma hizo hakutoathiri biashara.

Je kama ninatumia Windows XP, kompyuta yangu itaendelea kutumika?
Jibu ni ndiyo ila kuwa makini. Kusitishwa kwa huduma kwa Windows XP hakumaanishi kuondolewa kwa XP toka kwenye kompyuta yako, bali ni kutoweza pata huduma, hivyo Windows iliyopo kwenye komputa yako itaendelea kutumika kama kawaida, ila kuanzia sasa uhakika wa usalama wako utaendelea kupungua siku hadi siku.
Chanzo  mtandao  wa  dudumizi
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright Daniel Blog in Contemporary News
Back To Top