Kamati ya Kudumu ya Hesabu za Serikali Kuu (PAC), imeiagiza
ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) kufanya ukaguzi
maalumu wa matumizi ya Sh13 bilioni, katika Mkutano wa Benki ya
Maendeleo Afrika (ADB) uliofanyika Mei mwaka 2012.
Uamuzi huo umekuja baada ya kubainika kwa matumizi
mabaya ya fedha hizo, yaliyofanywa na Hazina kwa ajili ya ununuzi wa
samani za ofisini na kompyuta ndogo 200.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Zitto Kabwe alisema
mbali na vituo hivyo, Hazina pia imenunua, seti za televisheni za
ukutani, mashine za kuchapishia karatasi, viti na makochi ya sebuleni.
Alisema ingawa vifaa hivyo vimenunuliwa kwa fedha
za Serikali, baadhi yake vimeachwa katika ukumbi wa Kituo cha Mikutano
cha Kimataifa cha Arusha, bila ya kuwapo kwa makabidhiano ya kisheria.
“Kamati imepata mashaka kuhusu matumizi ya Sh13
bilioni katika mkutano wa ADB, jambo lililotufanya tumuombe CAG kufanya
ukaguzi maalumu wa matumizi ya fedha hizi za Serikali,” alisema Zitto.
zaidi soma
zaidi soma
Post a Comment