Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU), Dk
Salim Ahmed Salim, amesema umahiri wa vikosi vya kulinda amani Darfur na
kwingine Afrika unatia shaka, kwani vinakabiliwa na upungufu wa
vitendea kazi ikiwamo zana za kisasa.
Kauli ya Dk Salim inakuja ikiwa ni siku chache
baada ya kuuawa kwa wanajeshi saba wa Tanzania waliokuwa wakitumikia
Vikosi vya Kulinda Amani vya Umoja wa Mataifa na Afrika (Unamid).
Wanajeshi hao waliuawa wakiwa katika majukumu yao
na kundi la Wanamgambo, linalodaiwa kuiunga mkono Serikali ya Rais Said
al-Bashar la Janjaweed.
Dk Salim alisema himizo la kutaka kubadilishwa kwa
kifungu cha sita kwenda saba, liende sanjari na zana za kisasa ambazo
waasi hao wanatumia ikilinganishwa na walinzi wa amani wanaotumia silaha
za kawaida.
Chanzo:http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Walinzi-wa-amani-Darfur-wadaiwa-/-/1597296/1925656/-/cgb97e/-/index.html
Chanzo:http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Walinzi-wa-amani-Darfur-wadaiwa-/-/1597296/1925656/-/cgb97e/-/index.html
Post a Comment