Social Icons

Loading...

Ubalozi Marekani waipongeza TCCL kwa umakini

Serikali ya Marekani imeipongeza Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL, kwa kazi nzuri ya kusimamia mawasiliano wakati wa ziara ya Rais Barrack Obama wa nchi hiyo mwanzoni mwa mwezi huu.
TTCL ilipewa dhamana ya kusimamia mawasiliano yote tangu kufika kwa kiongozi huyo hadi kuondoka.
Ofisa Ubalozi wa Marekani nchini, Jeff Shrader alitoa pongezi hizo alipoongoza ujumbe wa maofisa wa ubalozi huo kutembelea makao makuu ya TTCL na kuzungumza na viongozi na wafanyakazi waliohakikisha kuwa sekta ya mawasiliano inakwenda vizuri na kwa ufanisi.
Ujumbe huo wa Marekani umeahidi kutoa vyeti kwa kutambua mchango wa TTCL na wafanyakazi wake hivi karibuni.Mkuu wa Masoko na Mauzo wa TTCL, Peter Ngota aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuwa kampuni hiyo imepata faraja kubwa kwa kupata mrejesho huo kutoka Serikali ya Marekani.
“Tumepata faraja…hii inaonyesha uwezo wetu kitaaluma na ubora wa vifaa tulivyonavyo katika kutoa huduma za mawasiliano,” alisema.
Alisema kuwa TTCL ilipewa sifa hasa kutokana na utaalamu, uchapaji kazi na weledi ulioonyeshwa na wafanyakazi wa kampuni hiyo kwa timu ya Wamarekani waliokuwa wakifanya kazi nayo.Ngota alisema kuwa kampuni hiyo itaendelea kufanya juhudi kuhakikisha inatoa huduma bora za kimataifa wa mawasiliano nchini.
Kampuni hiyo ya simu inaendesha na kusimamia mkongo wa taifa wa mawasiliano kwa niaba ya Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.
Mkongo huo unalenga kuwezesha matumizi ya Tehama katika sekta mbalimbali hapa nchini kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright Daniel Blog in Contemporary News
Back To Top