Meli kubwa kutoka China tayari imetua katika Bandari ya Mtwara
kwa ajili ya kushusha mizigo ya mabomba ya gesi ili kuanza kwa kazi ya
ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam.Mmoja wa watumishi ndani ya Bandari ya Mtwara
ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini, alisema zaidi ya magari 20
yanatakiwa kupakua mzigo wa mabomba zaidi ya 4,000 kutoka bandarini
hapo na kusafirishwa kwenda Kiranjeranje Lindi kwa ajili ya zoezi zima
la ujenzi wa bomba hilo.
“Hayo magari mliyoyaona ni miongoni mwa zaidi ya
magari 20 yanayokuja kupakua mzigo wa mabomba ambayo ni zaidiya 4,000
kwa ajili ya kuyapeleka maeneo mbalimbali ikiwemo Kiranjeranje Lindi kwa
ajili ya kufanikisha zoezi la ujenzi wa njia ya kusafirisha gesi,
upakiaji unaendelea hapa Mtwara na Dar meli inapakuwa mzigo ili
kupelekwa kwenye maeneo husika na upakuaji kwa mikoa yote unaendelea kwa
amani,” alisema.Akizungumza na gazeti hili mmoja wa madereva wa
magari maalumu kwa ajili ya kupakua mzigo wa mabomba,alisema wametokea
Dar es Salaam na hii ni zabuni maalumu waliyoipata kwa ajili ya
maandalizi ya kupokea mizigo na kupeleka yanakotakiwa hapo baadaye
baadaye baada ya kukabidhiwa kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
Chanzo : http://www.mwananchi.co.tz/-/1597570/1916578/-/104vy0r/-/index.html
Chanzo : http://www.mwananchi.co.tz/-/1597570/1916578/-/104vy0r/-/index.html
Post a Comment