HUKU Chama Cha Mapinduzi (CCM), kikiwa kimeweka bayana kwamba
hakiungi mkono Serikali tatu kama Rasimu ya Katiba inavyoonyesha, Waziri
wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe ameibuka na kusema endapo Mabaraza
ya Katiba yatawasilisha hoja za kuikubali, kuna uwezekano mkubwa wa
Uchaguzi Mkuu wa 2015 kukwama.
“Uwepo wa Serikali tatu utafumua mfumo mzima wa
utendaji ndani ya Serikali. Hatuwezi tena kufanya uchaguzi wa Rais na
wabunge 2015, hatuwezi kufanya chochote nje ya Katiba ya Serikali Tatu
kwa kuwa kinachofuata ni kuunda Katiba nyingine inayohusiana na Serikali
tatu.“Kama tutafanya uchaguzi, utafanyika kwa taratibu
zipi, ipi itakuwa mipaka ya marais wa Serikali tatu, makamu na mawaziri
wakuu, mfumo wa Mahakama, Tume ya Uchaguzi, utendaji wa Bunge na
wabunge, yako mengi, sasa mpaka hayo yaingie kwenye Katiba,” alisema
Chikawe juzi Dar es Salaam.
Alisema lazima CCM isimamie suala hilo kwa kuwa
kukubali Serikali tatu kutaua Muungano ambao sehemu kubwa unalindwa na
chama hicho tawala.
“CCM wamejipanga kama baraza na kusimamia hili la
Serikali mbili ambalo lengo ni kuulinda Muungano. Litakapokuja hili la
Serikali tatu, lazima Muungano uparaganyike,” alisema.Hata hivyo, kauli hiyo ya Waziri Chikawe
inakinzana na ile aliyoitoa Juni 4, siku moja baada ya Tume ya
Mabadiliko ya Katiba kutangaza hadharani Rasimu hiyo.
Post a Comment