Social Icons

Loading...

Simu zisizosajiliwa mwisho 31 Mei 2013.

Mamlaka ya Mawasilino Tanzania, TCRA, imesema watumiaji wa simu ambazo hazikusajiliwa, watakatiwa mawasiliano ifikapo Juni Mosi mwaka huu.
Tamko hilo lilitolewa jijiji Mbeya na Mkurugenzi wa Sheria na Leseni wa mamlaka hiyo, Elizabeth Nziga wakati wa semina kuhusu utekelezaji wa sheria mpya ya mawasiliano ya elektroniki na posta ya mwaka 2010 kwa wadau mbalimbali.Hiyo ni awamu nyingine katika mipango ya TCRA, kwani awali ilikuwa na kampeni za kuzima mitambo ya analogia nchi nzima na kuwataka wananchi kuingia katika mfumo wa dijitali ulioanzia katika Mkoa wa Dar es Salaam Desemba 31, mwaka jana.
Mikoa mingine iliyoingia kwenye mfumo wa dijitali ni Arusha, Tanga, Dodoma, Mbeya na Mwanza. Nziga alisema mamlaka hiyo inasisitiza kuwa hatua hiyo ni utekelezaji wa makubaliano kati yake na watoa huduma za mawasilino ya simu na kufikia usiku wa Juni Mosi, namba za simu ambazo hazikusajiliwa zitakoma. Mmiliki wake hataweza kuitumia kupiga wala kupokea siku.
Chanzo  gazeti  la mwananchi .
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright Daniel Blog in Contemporary News
Back To Top