Wakati leo Watanzania wakiungana na wenzao duniani kusherehekea
Sikukuu ya Wafanyakazi (Mei Mosi), wadau wa sekta mbalimbali nchini
wameitaka Serikali iwapunguzie kiwango cha kodi wanachokatwa (Paye).
Kwa kipindi kirefu sasa, wafanyakazi nchini wamekuwa wakilalamikia kodi kubwa inayotozwa kwenye mishahara na kiwango kidogo cha mshahara wenyewe. Kwa sasa kima cha chini cha mshahara ni Sh180,000 kwa mwezi.Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta), limeitaka Serikali kupunguza makato makubwa ya kodi na mifuko ya hifadhi ya jamii ambayo kwa kiasi kikubwa yamechangia wafanyakazi kupata kiasi kidogo cha fedha katika mishahara yao na kuishi katika mazingira magumu.
Katibu Mkuu wa Tucta, Nicolaus Mgaya alisema jana kuwa madai hayo ni ya muda mrefu, lakini hayajawahi kufanyiwa kazi, jambo ambalo limewafanya wafanyakazi wengi kukosa matumaini.
Alisema, awali walitoa mapendekezo ya kima cha chini cha mshahara kuwa Sh315,000 lakini mpaka sasa hakuna kilichofanyika na badala yake wamekuwa wakiongezewa kiasi kidogo kisichokidhi mahitaji.Mgaya alisema nyongeza ya mishahara imekuwa ndogo wakati makato ya kodi ni makubwa.

“Bado tunaendelea na malalamiko yetu ya nyongeza
ya mishahara na kupunguzwa kwa makato ya kodi kwa sababu Serikali
imeshindwa kutekeleza. Tutayawasilisha tena kwenye maadhimisho ya Siku
ya Wafanyakazi kesho (leo),” alisema Mgaya.
Alisema nauli zimepanda, lakini wafanyakazi bado wanalipwa mishahara duni, jambo ambalo linawafanya waendelee kuishi kwenye mazingira duni. Mbali na nauli, pia kuna tatizo la kupanda kwa mahitaji ya muhimu kama vyakula na malipo ya huduma za umeme na maji.
Hata hivyo, Mhadhiri wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), Bashiru Ally amevitaka vyama vya wafanyakazi nchini kupambana na mfumo badala ya kudai nyongeza ya mishahara pekee.
“Tanzania kuna mfumo wa unyonyaji, ili kuuondoa, vyama vya wafanyakazi vinatakiwa kuungana pamoja na kuwaunganisha wavuja jasho wengine kama mamalishe, madereva wa mabasi na wengineo ili wadai mfumo wa haki,” alisema Bashiru na kuongeza:
“Mfumo wetu ni wa kuwaongezea walionacho na kuwapunja wasionacho, wanatakiwa kuwa na mapambano ya muda mrefu ambayo yatawakomboa moja kwa moja, waige vyama vya wafanyakazi vya nchi jirani.”
Chanzo http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1762888/-/12b4awh/-/index.html

Post a Comment