Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa amesifia utawala wake kwa kuongoza
taifa bila ya kubaguana na amesikitishwa na matukio ya udini, ambayo
yanaashiria kuvuruga amani na utulivu wa Tanzania katika siku za
karibuni.
Akitoa salamu zake baada ya kusimikwa kwa Askofu
Mpya wa Jimbo Katoliki la Bukoba, Desdelius Rwoma, Mkapa alisema
anachojivunia ni kuheshimiwa na waumini wa madhehebu yote.
“Katika kipindi cha uongozi wangu, viongozi wa
madhehebu yote walikuwa wakinisisitizia kuwa sisi sote ni ndugu pamoja
na tofauti zetu za kiimani. Wakati wa utawala wangu nilijitahidi kwa
uwezo wangu wote kuwahudumia wananchi bila kuwepo kwa malalamiko ya
kubaguana katika jamii,” alisema Mkapa, ambaye aliiongoza Tanzania
kuanzia mwaka 1995-2005.
Mkapa alionya kuwa taifa limeacha misingi
aliyoiacha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, ambaye mara zote
alisimamia umoja wa taifa.
“Wakati wa utawala wangu nilijitahidi kwa uwezo
wangu wote kuwahudumia wananchi bila kuwepo kwa malalamiko ya kubaguana
katika jamii,” alisema.
Chanzo gazeti la mwananchi.
Chanzo gazeti la mwananchi.
Post a Comment