Man U 3 Aston Villa 0
MANU imetwaa ubingwa mara ya
20, huku mchezaji wake, Robin van Persie anayevaa jezi namba 20
akifunga mabao yote matatu dhidi ya Aston Villa katika Uwanja wa Old
Trafford.
Katika mchezo huo
uliochezwa Jumatatu usiku, Manchester United ilipata bao la kwanza
dakika ya kwanza na sekunde 23, kupitia kwa Robin van Persie aliyepokea
pasi maridadi kutoka kwa Ryan Giggs.
Mpira ulianzia kwa Wayne
Rooney, aliyetoa pasi kwa Antonia Valencia ambaye akiwa katika wingi ya
kulia alimpa pasi Rafael ambaye alitoa pasi ndefu kwa Giggs aliyempasia
van Persie.Dakika ya 13, Van Persie
alifunga bao la pili baada ya kupokea pasi ndefu kutoka kwa Rooney.
Baada ya kupokea mpira huo, Van Persie aliunganisha moja kwa moja na
kulifanya bao hilo kuwa miongoni mwa mabao bora msimu huu.
Dakika ya 33, Van Persie
alifunga bao la tatu baada ya Shinji Kagawa kumtengenezea pasi Giggs
aliyekimbia na mpira katika wingi ya kushoto na hakutaka kufunga
mwenyewe, badala yake akampa pasi Van Persie aliyemaliza kazi.
Si tu kwamba, Van Persie alifunga 'hat trick' hiyo, lakini alifikisha mabao 24 katika Ligi Kuu England.Mholanzi huyo, ambaye huvaa
jezi namba 20 ameifanya Manchester United kutwaa ubingwa wa 20. Huo ni
ubingwa wa 13 kwa Alex Ferguson ambaye alianza kuifundisha timu hiyo
tangu mwaka 1986.
Msimamo wa EPL fuatilia hapa http://www.premierleague.com/en-gb/matchday/matches.html
Post a Comment