WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna
Tibaijuka ameanzisha Wakala wa Kuendeleza Mji wa Kigamboni (KDA). Kwa
maana hiyo, mji huo hautakuwa tena chini ya mamlaka ya Manispaa ya
Temeke.Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam
jana, Profesa Tibaijuka alisema Serikali imeamua kuanzisha wakala huo
ili pamoja na mambo mengine, upange na kusimamia ujenzi wa mji wa kisasa
katika eneo hilo.“KDA imeanzishwa chini ya Sheria ya Wakala wa
Serikali ya 1997 ili iweze kuhakikisha mji unajengwa na unakuwa bora,”
alisema Profesa Tibaijuka.Alisema kutokana na kuanzishwa kwa KDA, kata zote
za Kigamboni, zitaungana na madiwani wake pamoja na mbunge wao watakuwa
wakikutana katika Baraza la Ushauri la KDA.“Kutakuwa na Baraza la
Kigamboni ambalo madiwani na mbunge wao wataingia humo kujadili
maendeleo ya mji huo na leo (jana), kutakuwa na kikao cha kwanza,”
alisema Profesa Tibaijuka.
Soma zaidi : http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1673740/-/11rnri0/-/index.html
Soma zaidi : http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1673740/-/11rnri0/-/index.html
Post a Comment