SAKATA la wakazi wa Mkoa wa Mtwara kupinga rasilimali ya gesi
ghafi asilia inayovunwa katika kijiji cha Msimbati mkoani humo kupelekwa
Dar es Salaam kwa njia ya bomba limepamba moto huku viongozi wa Chama
cha Wananchi (CUF), wakitumia hotuba na nukuu za kauli za Baba wa Taifa
Mwalimu Julius Nyerere kuhamasisha wananchi kumuenzi mwasisi huyo wa
taifa kwa kuupinga mradi huo.
Katika mkutano mkubwa uliofanyika jana Mtaa wa
Sinani mjini hapa viongozi wa CUFWilaya ya Mtwara Mjini, walikuja na
mbinu mpya ya kuhamsisha wananchi kuendelea na msimamo huo kwa kutoa
hotuba za nukuu ya kauli za Baba wa Taifa kuhusu mustakabali wa hali ya
maisha ya wananchi katika mazingira ya wachache kuwakandamiza wengi.
Saidi Kulaga, Katibu wa CUF Wilaya ya Mtwara mjini
alisema kinachotokea leo kwa wakazi wa mikoa ya Kusini ni kumuenzi
Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ambaye kwa nyakati tofauti
alinukuliwa akionya viongozi kuandamiza wengi.
Katibu huyo akisoma karatasi ya nukuu hizo kutoka
katika kitabu cha ‘Reflection on Leadership in Africa’ kilichopigwa
chapa na VUB University Press, 2000 alisema mwasisi huyo wa Taifa
katika kitabu hicho amenukuliwa akisema
Habari zaidi http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1663260/-/11r24q6/-/index.html
Habari zaidi http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1663260/-/11r24q6/-/index.html
Post a Comment