Social Icons

Loading...

Profesa Ndulu ataka BoT isiingiliwe na wanasiasa.

GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Benno Ndulu amependekeza Katiba Mpya iweke kinga ambayo itailinda benki hiyo ili ifanye kazi zake bila kuingiliwa na mambo ya kisiasa.
Aidha, amependekeza Katiba Mpya itenganishe mamlaka zinazotoa na zile zinazotumia fedha ili kila moja ifanye kazi zake kwa kujitegemea, huku pia akitaka kinga zinazolinda shughuli za kibenki zitambulike kikatiba na si kuwepo kwenye sheria za Bunge.
Alisema benki zinapaswa kutoa fedha kwa kiwango maalumu bila kuzizidisha kwa ajili ya kuimarisha uchumi.
Akizungumza Dar es Salaam jana muda mfupi baada ya kuwasilisha maoni ya BoT kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Profesa Ndulu alisema umefika wakati BoT ikajengewa uwezo wa kufanya shughuli zake bila kuingiliwa na wanasiasa.Profesa Ndulu alisema endapo BoT itawekewa kinga itakuwa na uwezo wa kufanya kazi zake vizuri zaidi.
Soma  zaidi :  http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1677998/-/11rqlh9/-/index.html
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright Daniel Blog in Contemporary News
Back To Top