RAIS Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa ameelezea
kufedheheshwa kwake na mgogoro wa gesi, huku akiwataka wananchi na wadau
wa maendeleo wa Mkoa wa Mtwara kusitisha harakati za maandamano na
mihadhara.Mkapa alitaka wakazi hao kuacha kulumbana na Serikali
kuhusu suala hilo, badala yake wajiandae kukaa meza moja nayo kutafuta
mwafaka kwa njia ya amani.
Katika tamko lake alilolitoa Dar es Salaam jana,
Mkapa alisema: “Fujo, vitisho, kupimana nguvu na malumbano siyo masharti
ya maendeleo.“Nikiwa kama mwana - Mtwara na raia mwema, mpenda
nchi, nimefedheheshwa sana na matukio haya ya siku za karibuni Mtwara.
Kwa sababu hiyo natoa wito kwa wadau wote wa maendeleo ya Mtwara,
kusitisha harakati hizi na maandamano na mihadhara.
“Badala yake wajipange kukaa pamoja katika meza
moja, kupitia historia, kutathmini mipango, kuchambua kwa kina mikakati
ya utekelezaji wake, hatimaye kufikia mwafaka wa ujia wa maendeleo.
Liwezekanalo leo lisingoje kesho.”Mkapa alisema mwenendo wa mazungumzo, maandamano
na mikutano ya hadhara inayoendelea mkoani Mtwara, inaelekea kuashiria
kuvunjika kwa amani hali aliyosema kuwa inajenga kutokuelewana kati ya
viongozi wa vyama vya siasa na Serikali, wananchi na vyama vya siasa na
wananchi na viongozi wa Serikali.
Soma zaidi : http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1672020/-/11rmwmu/-/index.html
Soma zaidi : http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1672020/-/11rmwmu/-/index.html
Post a Comment