WAZIRI Mkuu Raila Odinga na Makamu wa Rais, Kalonzo Musyoka
wamepewa ushindi wa awali katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika
Machi 4 nchini Kenya.
Kwa mujibu wa kura ya maoni ya Infotrak, iwapo
uchaguzi ungefanyika wiki hii, Odinga anayewania wadhifa wa kuongoza
nchi hiyo kupitia muungano wa Cord angeshinda kwa asilimia 51 ya kura.
Raila ambaye ni Waziri Mkuu katika Serikali
inayomaliza muda wake ndiye mgombea urais kupitia muungano huo, pamoja
na mgombea mwenza, Musyoka ambaye ni makamu wa Rais katika Serikali
hiyo.
Kwa mujibu wa matokeo ya utafiti huo uliofanywa na
kampuni ya Infotrak and Consulting, Raila na Kalonzo watapata asilimia
51 ya kura zote zitakazopigwa huku wapinzani wao wakuu, Uhuru Kenyatta
na William Ruto wanaowania wadhifa huo kwa tiketi ya muungano wa Jubilee
wakipata asilimia 39.
Hii ina maana kuwa iwapo mambo yakisalia yalivyo, uchaguzi wa urais hautaingia katika awamu ya pili.
Hii ina maana kuwa iwapo mambo yakisalia yalivyo, uchaguzi wa urais hautaingia katika awamu ya pili.
Kura hizo za maoni pia zinaonyesha mgombea urais
wa Muungano wa Amani, Naibu Waziri Mkuu, Musalia Mudavadi na Muungano
wa Eagle unaoshirikisha na Peter Kenneth na Raphael Tuju wanashika
nafasi ya tatu kwa kuzoa asilimia 3 ya kura hizo.
Wagombea wengine wanaoshiriki katika uchaguzi huo wa urais kwa tiketi za vyama vyao bila kuungana na vyama vingine,
Martha Karua na Professa James Ole Kiyiapi wamepata asilimia 0.3 na 0.1.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Angela Ambitho alisema kuwa katika utafiti huo, watu 1,500 walihojiwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Angela Ambitho alisema kuwa katika utafiti huo, watu 1,500 walihojiwa.
Alisema kura hiyo ilifanyika kabla ya Mudavadi
kuteuliwa rasmi kama mgombea urais wa muungano wa Amani unaoshirikisha
chama chake cha United Democratic Forum (UDF), Kanu na New Ford Kenya.
Utafiti huo ulifanyika kati ya Desemba 28 mwaka jana na Januari 2 mwaka huu katika kaunti 25 kwenye mikoa yote nchini.Chanzo Mwananchi
Post a Comment