HALI ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Jeshi la
Polisi (DCI), Kamishna Robert Manumba ni mbaya na amelazwa katika Chumba
cha Wagonjwa Mahututi (ICU), Hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam.Habari zilizopatikana jana zilieleza kuwa
Manumba amelazwa hospitalini hapo baada ya kusumbuliwa na maradhi
kadhaa, ikiwamo figo.
Taarifa za ndani kutoka Jeshi la Polisi zilisema jana kuwa tangu juzi, Manumba alikuwa hajitambui baada ya kuugua malaria ghafla na hali hiyo ilisababisha pia figo zake zote mbili kushindwa kufanya kazi.
“Alitakiwa kupelekwa nje ya nchi kwa matibabu,
lakini ilishindikana kwa sababu hajitambui, wakajaribu kumzindua,
ikashindikana,” kilieleza chanzo hicho cha habari ndani ya jeshi hilo.
Habari zaidi : http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1667476/-/11r4xlt/-/index.html
Habari zaidi : http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1667476/-/11r4xlt/-/index.html
Post a Comment