Dk Terezya Huvisa |
Dk Huvisa alifanya hivyo jana baada ya ziara ya kushtukiza akiwa na Naibu wake, Charles Kitwanga.
Waziri alitembelea hoteli hiyo ili kuona
utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na Kitwanga mapema mwezi huu,
alipofanya ziara katika viwanda na hoteli zilizoko pembezoni mwa bahari,
ili kuona mfumo wa majitaka.
“Nawataka kurekebisha mara moja mfumo huo wa majina kulipa faini kwa Baraza la Hifadhi na Uhifadhi wa Mazingira (Nemc),”alisema Dk Huvisa.
Dk Huvisa alifika hatua hiyo baada ya
kujiridhisha kuwa agizo lililotolewa na naibu wake wiki mbili
zilizopita, halijafanyiwa kazi.
Alisema hoteli hiyo itafungwa hadi hapo
itakapotekeleza agizo hilo na kuhakikisha kuwa majitaka hayatiririki
baharini kama ilivyo sasa.
Chanzo : http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1648058/-/11pwgxt/-/index.html
Chanzo : http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1648058/-/11pwgxt/-/index.html
Post a Comment